Sunday, February 17, 2013

SHUKRANI


 

 

 

SHUKRANI.

 

Asante ninaitoa,

Kwa wenzangu Tanzania,

Yangu kwa kujisomea,

Mchango nilioutoa,

Na akija kuwachiwa,

Mkufunzi anakuwa.

 

Kubwa linalotakiwa,

Kesho kuiangalia,

Sio kwa tuliokuwa,

Ila kizazi kijacho.

 

Nchi tukawaachia,

Tulivu iliyokuwa,

Pasina kununuliwa,

Mfukoni tukatiwa.

 

Kisha wakatuchezea,

Na kutufanzia ubaya,

Hadi tukakijutia,

Kiranga tulichoingia.

 

Yarabi namgeukia,

Hatari kutwepushia,

Katiba salama kuwa,

Ifae Watanzania.

 

Kisha funguo ikawa,

Mengi kwetu kufungua,

Daraja tukazijua,

Bora zitakazokuwa.

 

Hii yetu Tanzania,

Mfano kwa wengi ikawa,

Na wengine kulilia,

Waje na kujionea.

 

 

 
 
 

KUHUSU MTUNZI WA UTENZI:

Sammy W.I. Makilla ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) ambaye kwa sasa ni mtafiti/mwanafunzi kwa masomo ya juu zaidi ya shahada ya pili.

 

*   Mtunzi wa kitabu cha Tanzania: Chama Kimoja au Vyama Vingi? DUP, Dar es Salaam. Tanzania. 1992.

 

TANGAZO: Kwa wale wanaotaka kuchapisha utenzi huu kama kitabu cha kawaida tafadhali wawasiliane na mwandishi kupitia barua pepe: sammymakilla@hotmail.com au sammy.i.makilla@gmail.com.  Atakayewahi zaidi atakuwa wa kwanza kufikiriwa.

No comments:

Post a Comment