TULIPOPATA uhuru ilisemekana eti Uti wa mgongo wa taifa letu ni kilimo. Mkulima
na vijiji vimebadilika kidogo sana toka tupate uhuru. Ingawa tumejenga kiasi mijini lakini vijiji vimesahaulika.
Serikali na chama tawala vilipoua ushirika halisi na kuleta ushirika wa kisiasa
mkulima aliathirika vibaya sana.
Vijiji vya Ujamaa lilikuwa ni wazo zuri lakini watendaji wa serikali wakatumia fursa
hiyo kuchukua ardhi nzuri ya vijiji na kuwahamisha wakulima karibu na barabara
au kwenye maeneo yasikokuwa na rutuba hata kidogo.
Mamlaka nyingi z amazao zilizoanzishwa zilimnyonya na kumuibia zaidi mkulima
kuliko kumsaidia na wanasiasa taratibu wakavila na kuviua vyama vya ushirika.
Soko huria na siasa za kiliberali zilipoingia mkulima tu ndiye ambaye hakuruhusiwa
kuuza mazao au bidhaa alizozalisha nchi za nje. Na hadi wa leo soko la mkulima
limekuwa likivurugwa na serikali na wanasiasa. Tujiulize:
i. Kama tumekubali soko huru jambo hilo halimhusu pia mkulima;
ii. Kwanini tusimruhusu moja kwa moja mkulima kuuza mazao yake nchi
za nje kwa taratibu atakazopanga yeye na wenzake;
iii. Je, tukimhakikishia mkulima soko linalomlipa bei za kishindani kilimo
hakitafanikiwa;
iv. Je, VICOBA vya kilimo haviwezi kuendeshwa kwa namna ambayo sio
tu ni benki za kijamii, bali pia ni chombo cha bima na hifadhi ya mkulima (Social
security fund);
v. VICOBA vya wakulima vikishirikiana na benki za maendeleo ikiwemo
hiyo ya kilimo haziwezi kujipanga ili kuhakikisha wakulima wengi iwezekanavyo:
-wanakopeshwa matrekta;
-wanapata mbegu, mbolea na mahitaji yao mengine kirahisi na kwa namna
isiyowagharimu fedha yote kwa wakati mmoja;
-wanasaidiwa kutafuta masoko kabla ndani na nje ya nchi;
-wanafikishiwa hutuma muhimu vijijini kama vile maji, umeme na miundombinu
kwa kutumia pia idara ya VICOBA itakayopewa jukumu la utoaji huduma muhimu
kijamii na kibiashara;
-Je, VICOBA, Benki ya Kilimo, wafadhili na serikali itawasaidiaje wakulima kuwa
na nyumba bora na huduma zote muhimu ili pamoja na kilimo vijiji viweze
kuendesha pia biashara ya utalii wa vijijini na kilimo;
-Kila inapowezekana VICOBA na BENKI ya Kilimo visaidiwe uanzishwaji wa
viwanda vidgo vitakavyowasaidia wakulima kuuza unga sembe badala ya kuuza
mahindi; kuuza ngano iliyosagwa badala ya mali ghafi ya ngano; kuuza mchele
badala ya kuuza mpunga na kuuza mafuta ya kupikia badala ya kuuza alizeti na
nyonyo;
-Je, hivi wizara ya Kilimo na chakula inatakiwa iwe na wafanyakazi wanaoishi na
kuonesha mifano vijijini au wapunge upepo wa bahari kama sio wa bonde la
TAZARA?
-Na yote haya yatazungumzwa na nani kama sio mwakilishi halali na
anayetegemewa kuzungumza kinachotakikana kama sio mwakilishi wa
wakulima/wanavijiji;
Jitayarisheni, jiandaeni na kujihami na nguvu za hoja kuhusu umuhimu wa kuwa
na Baraza au Mkutano wa Kitaifa wa Katiba Mpya 2011 na wala sio Tume au
Kikundi cha wateuliwa wachache hata kama ni mawaziri, wabunge, majaji,
wanasheria na engineo kama hao, maana historia inaonesha wote hao hawawezi
kutetea maslahi yako wewe na kwamba mwamba ngoma ngozi lazima avutie
kwake au sio?
[1],2,3,4,5,6,7,8,9,10,11,12,13,
14,15,16,17,16,19,20,21,22,23
,24,25,26,27,28,29,30,31,32,3
3,34,35,36,37,38,39,40,41,42,
43,44,45,46,47,48,49,50.
HakiKatiba 2011:
WAKULIMA wetu sio wajinga. Wanasiasa waliotaka kuwageuza wakulima kuwa punda wao na kuchuma kupitia migongo yao badala ya wao kuwa uti wa mgongo wa taifa ndiyo zilizotufikisha hapa tulipo leo!
No comments:
Post a Comment