Friday, May 27, 2011

21. Mtafiti

PAMOJA na kutambua umuMWANAMICHEZOhimu wa Vyuo Vikuu na vyuo

vingine bado Tanzana iko nyuma sana katika kuwawezesha watafiti kuendesha

tafiti mbalimbali zitakazoweza kuboresha maisha ya Mtanzania.

Utafiti na Uendelezaji vitu na taasisi ni kitu muhimu sana katika jamii. Kutokana na

hili inafaa serikali yoyote kujipanga kwa namna ambayo saa zote walimu,

wahadhiri na maprofesa wa vyuo na vyuo vikuu wanakuwa wana utafiti au ushauri

fulani wanaotekeleza ili kutatua tatizo fulani lililopo au kuwafungua watu na serikali

macho kuhusu fursa zinazojitokeza na jinsi zinavyoweza kutumika ili kuinufaisha

nchi.

Sio hivyo tu, nchi hii na viongozi wamekithiri kwa kuwa wachache wa shukrani na

hasa pale wanapotumia mawazo au fikra za mtu fulani kutangaza, kufanya au

kuamua jambo fulani. Na hili linafanywa na watu wa chini mpaka viongozi wa juu.

KUna uwizi wa aina nyingi, lakini ni vyema pia kujua unaweza ukawa mwizi wa

mawazo ya mtu mwingine. Huu hauna tofauti na wizi mwingine na dhambi ya wizi

wa aina zote haitofautiani kwa maoni yangu. Kweli mtu anaweza asilipe fedha au

kumshukuru mhusika moja kwa moja, lakini ni uungawana na ustaarabu kwenye

hotuba au maandishi iwe kitabu au gazeti ijulikane ni wapi umelipata wazo hilo na

kwamba wewe siye mwasisi wake bali yupo mtu mwingine.

Ni dhahiri, tabia hii kadri inavyoendelea inaondoa kabisa imani na kuaminana kati

ya watu. Na funga na kufumbua utakuta tuna nchi ya matapeli na watu wa kuibiana

sio tu mawazo, bali hata vitu vingine pia na bado mtu akaona hajafanya kosa na eti

kafanya kitu cha halali kabisa.

Yapo mengi yanayowakatisha tamaa watafiti. Ipo mifano ya watafuta PhD.

wanaolipwa milioni 3 kwa miaka yote ya masomo, wakati wenzao hata nchi jirani

wanalipwa milioni 26 kwenda juu. Aidha, uwezo wa kununua vitabu na majarida ni

chini, uwezo wa kununua kompyuta nao nadra, maktaba zetu zimechoka,

upatikanaji data shida tupu, usafiri mashaka, mawasiliano mzigo na kadhalika.

Watafiti lazima wawepo katika Baraza la Katiba Mpya 2011, ili wahakikishe

kwamba kile wanachotaka kukifanyia Watanzania na nchi yao, nahitaji yao,

matarajio yao viwe ni vitu vinavyoeleweka na kuwekwa ipasavyo ndani ya Katiba

mpya,


WATAKAOCHANGIA bila uchama, ukabila, ueneo, udini, ubinafsi na ushawishi wowote toka kundi lolote ndani au nje ya nchi watastahili kupewa tunzo ya juu kabisa ya Kitaifa.

NI haki na wajibu wenu pia kuwaamsha, kuwafundisha na kuwaelekeza wananchi wengine nini wanachopaswa kufanza ili mahitaji yao ya msingi, dhiki, mapungufu kwao, kasoro zilizopo kwenye maeneo na maisha yao, haki na maslahi yao yote yaweze kupatikana kwa kutumia katiba na sheria za nchi na sio vinginevyo.

Ni muhimu pia wananchi kuelewa kwamba serikali ni kitu kinachodumu milele mpaka mwisho wa dunia lakini vyama vya kisiasa ni taasisi za kupita, leo vinaweza kuwepo na kesho visiwepo na vikaja vyama vipya kabisa madarakani.

No comments:

Post a Comment