MTANZANIA una haki ya wewe kuwa na mwakilishi katika chombo kitakachozungumzia na kisha kusaidia kazi ya kuandika katiba mpya. Katika wakati huu, wewe mwananchi, raia wa Tanzania unapanda cheo na kuwa ndiye mwajiri wa rais,makamu wa rais, mawaziri, wabunge na watumishi wote wa serikali. Kazi yangu katika mchakato huu ni kuwaambia viongozi hao kwamba: 'tunawataka mtutawale hivi na uwezo na sifa zenu ziwe hivi. Kinyume cha hivyo tutawafuta kazi..' endelea kurasa inayofuatia:
Friday, May 27, 2011
12. MWANAFUNZI.
MTANZANIA wewe ndiye unayemwajiri rais, mawaziri, wabunge na watumishi wa
umma. Na wewe ndiye mmiliki wa Katiba. Na katiba ni mchakato wa wewe
kuwaambia watawala waliopo na wajao unataka utawaliwe vipi na wao. Je, kuna
mtu mwingine anayeweza kuwasilisha ipasavyo unachokitaka kiwe, matakwa yako,
matarajio yako maslahi yako na ndoto ya Tanzania uitakayo na ile ya wewe
mwenyewe unachotaka kuwa kama sio mwakilishi wako anayeguswa na
yanayokugusa?
WANAFUNZI wa Kitanzania tokea chekechea wana haki kadhaa wanazozikosa nazo zinatambulika na kila mmoja wetu lakini ni kazi yao kuuelezea umma juu ya shida, dhiki, upungugu, dharau, unyanyasaji, kupuuzwa kwao na kutoshirikishwa kwao katika maamuzi na shughuli mbalimbali za kishule na jinsi ambavyo yote haya yakisahhishwa shule na vyuo nchini mwetu patakuwa ni eneo la utulivu, utafiti, ushauri, elimu na maarfia mapya wakati wote.
Kwanza, majengo na samani katika madarasa kwenye shule nyingi ni jambo linalostahili fungu maalum la bajeti kila mwaka kwa kuzingatia uchakavu na uharibifu wa vitu unaotokea kila mwaka kama sio kila mwezi.
WATANZANIA tuna kila sababu ya kuikataa tabia inayojitokeza na kujijenga Afrika ya kuwatumia polisi na wanajeshi wetu kuwapiga, kuwatia ulemavu au hata kuwaua baba zao, mama zao, ndugu zao, kaka zao, dada zao, watoto wao, rafiki na jamaa zao. Na hili linataka demokrasia kamili, pana, refu na ya kina lakini wakati huo huo ikikataa usiri, uozo, uongo, ulaghai na kuwadanganya wananchi na rushwa, wizi na ufisadi unaolindwa na kuenziwa na chama cha kiasiasa ili kiendelee kubaki madarakani milele.
HakiKatiba 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment