MIAKA kadhaa Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi za mwanzo kabisa Afrika
kuwa na Kitivo cha Uhandisi kwenye Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Vyuo kadhaa vya ufundi ukiachilia mbali vile vya VETA vilivyokuja baadaye pia
vilianzishwa kwa madhumuni kama hayo.
Katikati hapa sera na mwelekeo wa kisiasa umeua au kulemaza sana taasisi zote
ikiwmo viwanda, maabara, vyombo vya usafirishaji na uchukuzi kiasi ambacho
mustakabali wa wahandisi na mafundi wengine uko mashakani.
La kusikitisha ni kuwa Mhandisi wa Kitanzania hadi wa leo hajaweza kutengeneza
hata sindano achilia mbali pasi, balbu, pampu ya maji, baiskeli, redio, televisheni
achilia mbali mashine na mitambo inayotakikana kwa uzalishaji hili au lile.
Serikali hii imebweteka mno kuhusu suala la uhandisi na nafas yake katika kutumia
kwa vitendo sayansi, teknolojia na teknohama katika miaka hii ambayo kuna
wahandisi tele na maprofesa na wahadhiri wa uhandisi kwenye nchi kama Urussi,
Ulaya ya Mashariki , Korea Kusini, Japani na kwingineko ambao wangelipenda
sana kuja kukutana na changamoto zetu za kuwa taifa linaloweza kutengeneza
matrekta madogo kwa makubwa yake lenywe; baiskeli zake lenyewe; pikipiki lake
lenyewe; magari yake lenyewe; reli na treni zake lenyewe; meli na feri zake;
maturbine yake ya gesi na maji lenyewe; barabara zake lenyewe; viwanja vya
ndege vyake lenyewe; bandari zake lenyewe za baharini au ziwani au nchi kavu;
pampu zake kubwa kwa ndogo za maji lenyewe; mitambo na mashine kwa
viwanda vyake vidogo lenyewe na kadhalika.
Ni muhimu suala hili lijitokeze sana katika Uandikaji wa Katiba mpya ili kujenga
baada ya hapo mazingira mapya yatakayokuwa mazingira rafiki na azizi katika
kufanikisha ndoto hizo hapo juu.
Na hili haliwezekani bila wahandisi wetu wa leo kuja kuzungumza na kuandaa
mazingira ambayo wahandisi wa kesho watajiona ni zawadi kwa taifa na sio mzigo
usio na faida. Ushiriki wa wahandisi katika baraza au mkutano wa kitaifa wa katiba
kwa hivyo ni kitu adhimu na kinachohitajika sana.
Jitayarisheni, jiandaeni na kujihami na nguvu za hoja kuhusu umuhimu wa kuwa
na Baraza au Mkutano wa Kitaifa wa Katiba Mpya 2011 na wala sio Tume au
Kikundi cha wateuliwa wachache hata kama ni mawaziri, wabunge, majaji,
wanasheria na engineo kama hao, maana historia inaonesha wote hao hawawezi
kutetea maslahi yako wewe na kwamba mwamba ngoma ngozi lazima avutie
kwake au sio?
Makampuni yetu ya maji, umeme, viwanda na miradi mingine kama hiyo haitafufuka na kuendelea bila kuwashirikisha Wahandisi na kuwaachia kuwa viongozi wa sekta hiyo. Siasa zinaharibu zaidi maendeleo ya viwanda na siasa hazifai katika sekta ya viwanda.
HakiKatiba DEMOKRASIA ya kweli huheshimu mgawanyo wa madaraka na kazi. Wanasiasa wanaojitia ni mabingwa na maprofesa wa kila kitu hawatatufikisha mbali.
No comments:
Post a Comment