Friday, May 27, 2011

34. MWANAMICHEZO, FIZIKALI.

NCHI yenu imedorora kupitta kiasi katika michezo na baadhi yenu sasa mmeanza kutumika kama punda wa kubeba madawa ya kulevya, je, nini kifanyike kuinusuru michezo na sanaa katika nchi hii?

i. Michezo mashuleni iboreshwaje ili kuhakikisha kuna kuna shule zinazospeshalaizi katika michezo angalau kila kata kwa msingi na sekondari ili kuandaa maprofeshenoo wa siku zijazo, walimu wa michezo, viwanja vya michezo, mashindano wakati muafaka, lishe bora, usafiri salama na malezi na ulinzi muafaka wa wanamichezo makambini?

ii. Je, tutegemee mtu mmoja kuendeleza michezo au kuwe na taasisi, sera tumikifu, mifumo inayofanya kazi, bajeti/fedha, viongozi bora na safi na misaada ya hali na mali toka serikalini, mikoani na wilayani. Aidha, matumizi bainifu na ya wazi ya misaada toka ndani na nje ya nchi toka mashirika na watu binafsi?

iii. Kwanini michezo na sanaa zisiwekwe chini ya Mamlaka zinazojitgemea, yaani, zisiwe ni sehemu ya wizara bali ni taasisi huru zinazowezeshwa na kulindwa na serikali na lengo la kuja kujiendesha zenyewe kutokana na mapato yake ya ndani na nje ya nchi kutokana na ushiriki wake katika mashindano na shughuli mbalimbali? Kwa mfano, biashara kuuza wachezaji soka nchi za nje isipoangaliwa inaweza kuwa ni uuzaji watu na ikaja wanufaisha watu wachache tu na sio nchi nzima kwa ujumla?

iv. Tufufuaje michezo iliyokufa au yenye hatari ya kufa kama vile riadha, ngumi, mbio za magari, mbio za pikipiki, mbio za baiskeli na mengineyo kama hayo?

v. Tuwekeje uwazi katika malipo au fedha anazopata mchezaji ili wasiendee kudhulumiwa na viongozi wa michezo, mapromota, wauzaji wanamichezo na wasanii, makocha na walimu wa michezo na sanaa ? Na hatimaye wanamichezo na wasanii wapate mapato ya kuridhisha yatakayowachochea kufanya vizuri zaidi na kuwavuta wengine kwenye michezo na sanaa?

Je, mwanamichezo na msanii kuna mtu atakayewakilisha kikamilifu ndoto yenu hii na kutetea maslahi yenu kikatiba kama siyo nyie wenyewe kwa kuhakikisha sheria mama, yaani, katiba, inaweka wazi juu ya masuala yote muhimu yanyohusu michezo na sanaa na jinsi gani wanamichezo na wasanii wanavyoweza KUJIAJIRI NA KUTAJIRIKA kutokana na vipawa au vipaji vyao?

Tunapozungumzia mafanikio ya sekta hii hakika tunazungumzia mabilioni ya shilingi yatakayotiririka kwenye hazina ya taifa na kuipunguzia nchi umaskini, elimu duni na tiba zisizoridhisha za afya. Aanayechezea namna hii shilingi chuoni hivi anafaa kuwa kiongozi wa Watanzania?

Ni lazima tuoneshe njia kwa kushiriki katika Baraza la Katiba Mpya ili serikali iwayo ijue tunataka sekta yetu ya muziki na usanii iendeshwe vipi na sio kwa huruma na msaada wa huyu au yule ambaye hatakuwa nasi au na kizazi chetu kijacho daima.

No comments:

Post a Comment