MTANZANIA wewe ndiye unayemwajiri rais, mawaziri, wabunge na watumishi wa
umma. Na wewe ndiye mmiliki wa Katiba. Na katiba ni mchakato wa wewe
kuwaambia watawala waliopo na wajao unataka utawaliwe vipi na wao. Je, kuna
mtu mwingine anayeweza kuwasilisha ipasavyo unachokitaka kiwe, matakwa yako,
matarajio yako maslahi yako na ndoto ya Tanzania uitakayo na ile ya wewe
mwenyewe unachotaka kuwa kama sio mwakilishi wako anayeguswa na
yanayokugusa?
Ni jukumu la serikali kuwa na mipango, mikakati na sera sahihi zinazohakikisha
kwamba taasisi, zana na vifaa vyote unavyohitaji wewe kama mwanasayansi japo
sio vya kutufikisha mwezini vinakuwepo.
Ni jambo la kutia aibu kwamba katika miaka hii tuna shule za sekondari na vyuo
ambavyo havina hata maabara ya kemia, bayalojia, fizikia na uhandisi wa kemikali
na mambo kama hayo.
Mwanasayansi wetu ambaye mara nyingi ni mtafiti pia ni rasilimali adimu.
Tukiacha kuwapatia vitu wanavyohitaji ili kufanya kazi zao inakuwa ni rahisi sio
wao kukimbia bali serikali na wansiasa wetu kuwafukuza wakaenda kuishi na
kufanya kazi nchi za nje tena kwa maslahi bora zaidi mara 10 ya yale ya hapa
nyumbani.
Huruma kwa watu wao na uzalendo wao, hata hivyo, tukiacha kuwafanyia kile
wanachokitrajia huishia tu pale maslahi ya watoto na familia zao yanapokosekana.
Hakuna mtu mwingine anayeweza kuwasaidia ili Katiba iainishe sio tu wajibu wao
kwa jamii bali pia haki na kuhitajika kwao na nchi na watu wake kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.
WATAKAOCHANGIA bila uchama, ukabila, ueneo, udini, ubinafsi na ushawishi wowote toka kundi lolote ndani au nje ya nchi watastahili kupewa tunzo ya juu kabisa ya Kitaifa.
NI haki na wajibu wenu pia kuwaamsha, kuwafundisha na kuwaelekeza wananchi wengine nini wanachopaswa kufanza ili mahitaji yao ya msingi, dhiki, mapungufu kwao, kasoro zilizopo kwenye maeneo na maisha yao, haki na maslahi yao yote yaweze kupatikana kwa kutumia katiba na sheria za nchi na sio vinginevyo.
Ni muhimu pia wananchi kuelewa kwamba serikali ni kitu kinachodumu milele mpaka mwisho wa dunia lakini vyama vya kisiasa ni taasisi za kupita, leo vinaweza kuwepo na kesho visiwepo na vikaja vyama vipya kabisa madarakani.
No comments:
Post a Comment