JE, unajua wewe ndiye MMILIKI WA KATIBA na ndiye unayemwajiri rais, makamu wake, mawaziri na serikali nzima ?
USAFIRI wetu ndani na nje ya mikoa bado unatatiza na hauridhishi kwa mabasi, treni, ndege na meli au feri.
Hakuna aliye katika biashara ya usafiri anayetaka kutoa huduma mbovu au kupata hasara. Ipo haja ya katiba kuweka wazi muundo na mfumo unaohitaji katika usafiri na jinsi watu watakavyoweza kuwekeza katika sekta hii ili wanufaike wao na nchi nayo inufaike kwa usafiri bora na salam.
Barabara na mabasi yetu yanaweza kuwa kivutio kikubwa kwa wenyeji na wageni na safari zikawa raha badala ya karaha kama serikali inauona wito huu.
Reli ya Kati na Tazara zikipata muwekezaji siriazi anayejua akiwekeza atakuwa na faida ya muda mrefu Tanzania na sio wawekezaji uchwara wanaokotwa sijui na nani huko nje tunaweza kabisa kuwa na mfumo mzuri wa safari za relwe kiasi cha kuwa pia ni kivutio cha aina yake hapa nchini. Wadau wa sekta hii wanaamini kwamba katika miaka hii ambayo kuna wahandisi kabakaba wasio na kazi duniani relwe yetu ikigawanywa kwa vipande vinvyopita kila mkoa basi kila mkoa utaweza kwa namna fulani na msada kidogo toka serikalini na wanaoipenda Tanzania hatua kwa hatua kujenga pembeni ya reli ya sasa reli nyingine na hviyo kuwa na reli pacha ambazo baada ye moja itatumika tu kwenda na nyingine kurudi na hivyo kuharakisha kasi yetu ya usafiri na hasa treni hizo zitakapoanza kutumia umeme.
Ile reli ya Dar es salaam-Tanga na Tanga-Arusha inaweza ikafufuliwa kwa aina yake kwa kuifanya kuwa ni Northern Circuit Fantasy Tourism Railways.
Treni za njia hii zitakuwa na vyumba vizuri vya kulala, migahawa/mahoteli, baa, hospitali, yumba vya kamari na maonesho, muziki na starehe nyingine Wageni wanazopenda katika njia nzima. KIla kijiji au mji utakaoanzisha na kuendeleza vivutio vya utalii vinavyovutia kikweli kweli vitapewa nafasi ya wageni kukaa kwa muda au siku fulani hapo kabla hawajaendelea na
safari. Na katika mbuga za wanyama treni itakakopita watasimama kwa muda kutazama na kuchukua picha wanazotaka.
Maana uzuri na faida ya treni hii ya Dar es salaam-Arusha ni kuwa pamoja na kuchukua watalii hao nyuma inaweza ikabeba mabogi na mabehewa kadhaa ya abiria na mizigo.
Je, haya SUMATRA wameshafikiria? Na kama bado baada ya hapa je, sasa wanaipata picha na wanaweza kwa ushirikiano na wengine ndani na nje kuigeuza ndoto yangu hii kuwa kitu cha kweli?
Maziwa yetu na mito yetu mingi ambayo inaweza kuchukua feri kama sio meli kubwa tu hayana usafiri salama, mororo na laini na unaoweza kumfanya mgeni daima kukumbuka safari yake. Je, serikali kwanini imeshindwa kurahisisha kuwepo kwa feri, meli na boti za kasi katika Ziwa Victoria, Tanganyika, Nyasa na mito ya Ruvuma, Rufiji, Malagarasi kuwa ni maeneo ya safari na uchukuzi mizigo wa uhakika ? Hakuna wawekezaji ndani au nje au ubabe, rushwa, mabavu na maslahi binafsi yanatawala hapa? Ni muhimu kuchokonoa mzinga wa nyuki tuone kama tutaumwa au tutakula asali.
Kwa upande wa anga sekta ya umma imevurunda kabisa. Je, matatizo yasiyokwisha ya ATC pamoja na hoja za baadhi ya Wabunge kwamba lifufuliwe kweli zina maana yoyote?
Ninaamini, bado tunahitaji Usafiri wa ndege lakini plus angalau Meneja Mkuu wa shirika hilo akiwa mtu mwenye elimu, ujuzi, maarifa na uzoefu wa kuendesha shirika la ndege hata akiwa ni wa kutoka Ethiopia, Misri, Qaar, Uingereza, Ufaransa na kwingineko na akaachiwa kuwa na timu yake lakini yenye mameneja wazawa wanafunzi chini yao ili kuhakikisha kuwa shirika hilo likianza linaanza kwa mipango sahihi na mikakati maridhawa itakayolifanya lisishinndwe tena pamoja na matatizo ya dunia kiuchumi kwa sasa.
Aidha, serikali isione gere katika kusaidia mashriika binafsi ya ndege nchini kwa kurarahisishia kwanza kodi na masharti mbalimbali hadi hapo mashirika hayo yatakapokuwa na kukomaa na faida zake kuonekana waziwazi.
Hakika kuna kitu cha kujivunia katika kuona mnapeperusha ndege yenu wenyewe lakini sio katika hasara bali kwa faida na uridhishwaji mkubwa wa abiria wakati wote. Air Tanzania -irudi hewani, lakini ikiwa na uongozi mpya na matumaini mapya. Kushindwa mara mbili tatu kusiwe sababu ya kukata tamaa. Tatizo letu ni watu, fedha na sera. Na hivi vinaweza kubadilishwa na kuchanganywa hadi fomula inayowezesha Ethiopia kutamba na ndege zao ikapatikana. Ninaamini wapo Watanzania wengi tu ambao ni marubani na wafanyakazi katika mashirka ya ndege ya nje, ukiachilia mbali wana-Afrika mashariki wengi tu kwa ujumla wao ambao wanweza kutushauri ya msingi na ya maana sana katika hili.
Usafiri wetu mjini unaoweza ukawa unaotamanisha na kuwapumbaza wageni. Usafiiri wetu unaweza ukawa bora na wa maana na hasa sekta hii ikishirikiana na SUMATRA na TANROADS katika kugeuza barabara zetu za kitaifa kuwa pia kivutio kwa wenyeji na watalii na sio tu kivutio cha ajali, malumbano na kukorofishana kila siku.
No comments:
Post a Comment