JE, unajua wewe ndiye MMILIKI WA KATIBA na ndiye unayemwajiri rais, makamu wake, mawaziri na serikali nzima ?
MTANZANIA wewe ndiye unayemwajiri rais, mawaziri, wabunge na watumishi wa umma. Na wewe ndiye mmiliki wa Katiba. Na katiba ni mchakato wa wewe kuwaambia watawala waliopo na wajao unataka utawaliwe vipi na wao. Je, kuna mtu mwingine anayeweza kuwasilisha ipasavyo unachokitaka kiwe, matakwa yako, matarajio yako maslahi yako na ndoto ya Tanzania uitakayo na ile ya wewe mwenyewe unachotaka kuwa kama sio mwakilishi wako anayeguswa na yanayokugusa?
Kwa kuwa wanasiasa wetu wamejigeuza mabingwa na wataalamu wa kila kitu na kuingilia sekta kama hii yenu ya viwanda na uzalishaji mali kwa ajili ya kuuza ndani na nje mambo mengi yamevurugika.
Sera za serikali za upatikanaji umeme na nishati mbadala; miundombinu maridhawa; maji; mali ghafi; huduma muhimu za kijamii; mahitaji ya msingi ya wananchi wote; wafanyakazi wenye elimu na ujuzi; mameneja wazoefu na watundu wa kujaribu; masoko ndani na nje ya nchi; watu wabunifu na wavumbuzi; na wataalamu wa mambo mbalimabli zikiwa mbovu hukatisha tamaa, kuwavunja imani na kuwakimbiza wawekezaji wawe wa ndani au wa nje, na hususan wanaotaka kuwa na viwanda na miradi mikubWA katika nchi husika. Serikali inayofanikiwa ni ile inayoweka vipaumbele na kutambua ifanye lipi kwanza na yepi yafuate baadaye. Wale wanaochanganyikiwa na kutaka kufanya kila kitu kwa wakati mmoja huishia kuchanganyikiwa zaidi na kuibomoa badala ya kuijenga nchi.
Ieleweke nchi inaweza ikajaliwa kuwa na viongozi wa kisiasa ambao sioi lazima wawe ni viongozi wa mambo mengine. Nikisema hivyo nina maana kwamba nchi inahitaji pia magwiji, wataalamu, wajuzi na watu wazoefu katika sekta mbalimbali nao kuwa viongozi kwenye maeneo yao maana wao ndio waliosomea kwa undani maswala husika na hata wao wasipokuwa viongozi bado ni muhimu serikali na viongozi wa chin hadi juu kutafuta ushauri wao kila jambo linalohusu maeneo yao linapowafikia viongozi hao liwe kama changamoto au tatizo au fursa ya kiuchumi, kijamii, kiutamaduni, kimichezo au kiteknolojia.
Viwanda vinakufa kwa sababu viongozi wetu walijifanya wanajua kila kitu na hawakutaka ushauri wa mtu yeyote na hasa ukizingatia kulikuwa na teni pasenti nyingi zinazotoka kwa waliokuwa wakibinafsishiwa viwanda hivyo bila michakato yakinifu yakujua uwezo wa wahusika au la.
Tunahitaji viongozi wa Kiuchumi muichukue nafasi yenu iliyoporwa na viongozi wa kisiasa ili muiweke nchi kwenye njia sahihi.
KUWEPO kwenu katika Baraza la Kitaifa la Kuandika Katiba mpya ni muhimu ili muweze kuhakikisha 'visheni' ya pamoja ya wanaviwanda na 'micheni' zenu tofauti zinakuwemo kwa kifupi katika katiba na baadaye kwa ukamilifu wake katika sheria na sera zinazohusu viwanda na uzalishaji mali nchini.
No comments:
Post a Comment