Friday, May 27, 2011

42. MWENYE NYUMBA.

MWENYE NYUMBA una haki zako na unazijua. Na ili uzitetee na kuzitolea haja usikose mwakilishi wako katika Baraza la Katiba Mpya 2011.

Nyumba yako ni rasilimali. Hatimilki ni haki yako na huna sababu ya kuhonga ili uipate. Na huduma muhimu katika nyumba kwa hali ya dunia ya sasa sio maji na umeme tu. Ni lazima uwe na barabara safi na sio jalala nje ya nyumba yako linalitwa barabara.

Kadhalika TANESCO haina haki ya kuacha nguzo zilizoegema au nyaya zinazoning'inia karibu na nyumba yako. Au shrika lliwalo la maji kuacha maji yanavuja ovyo pembeni ya nyumba yako.

Serikali za mitaa hazina haki kabisa ya kukudai wewe kodi hii au ile kama zinashindwa kuhakiksha nyumba yako imeunganishwa na mfumo wa maji safi na pia maji taka. Na kwamba upo wakati wote utaratibu wa kunyonya vyoo na sio mvua zikinywesha jirani yako anafungulia kinyesi toka chooni mwake kinachoelea mbele ya nyumba yako. Hilo halikubalik.

Unahitaji pia kuwa na miundo mbinu ya simu na intaneti hadi ndan ya nyumab yako ili isiwe 'dili' kuwa na wapangaji kutoka nchi za nje pia katika nyumba yako.

Ni wewe tu au mwakilishi wako akishiriki katika Baraza au Mkutano wa Katiba Mpya na wala sio rais, waziri, mbunge au mkuu au yule anayeweza kuzungumzia adha na masahibu yako kwa ufasaha.
Jitayarisheni, jiandaeni na kujihami na nguvu za hoja kuhusu umuhimu wa kuwa na Baraza au Mkutano wa Kitaifa wa Katiba Mpya 2011 na wala sio Tume au Kikundi cha wateuliwa wachache hata kama ni mawaziri, wabunge, majaji, wanasheria na engineo kama hao, maana historia inaonesha wote hao hawawezi kutetea maslahi yako wewe na kwamba mwamba ngoma ngozi lazima avutie kwake au sio?

No comments:

Post a Comment