MPANGAJI una haki kabisa ya kukaa kwenye nyumba iliyojengwa na ikawa imekamilika kwa kila hali na yenye huduma bora na safi za choo, maji, umeme, utupaji taka na kadhalika.
Unastahili kulipa kodi inayoendana na ukubwa wa chumba au nyumba unayopanda. Aidha, pia eneo lilipo nyumba hiyo, hali ya mandhari na upya au uchakavu wa jengo unachangia kuamua pango halali kwa upande wako.
Mnapata shida nyingi kat yenu na wapangaji wenzenu; mwenye nyumba, mke wake na jamaa zake. Lakini pia mna haki ya kuishi kwa staha na amani toka kwa mwenye nyumba na jirani zake.
Hali kadhalika, unapoishi wewe kwa kuwa ni eneo la makazi na sio la starehe au burudani hapatakiwi kuwepo karibu mabaaa, magesti au mapabu au madisko yatakayosababisha makelele na usumbufu kwako na kwa familia yako.
Unapokuwa na matatizo binafsi ukashindwa kulipa pango basi mwenye nyumba atakufuza kama mnyama mwenye ugonjwa wa hatari zaidi ya ebola.
Haya yote, yatafanyika tu endapo na wewe au mwakilishi wako atashiriki katika Bunge la Katiba Mpya Tanzania 2011 na kuviweka wazi na bayana vifungu vyote kuhusu mahusianao yako wewe na mwenye nyummba wako iwe mtu binafsi, taasisi au wakala serikali.
No comments:
Post a Comment