Friday, May 27, 2011

13. MTUMISHI WA UMMA.

MTANZANIA wewe ndiye unayemwajiri rais, mawaziri, wabunge na watumishi wa

umma. Na wewe ndiye mmiliki wa Katiba. Na katiba ni mchakato wa wewe

kuwaambia watawala waliopo na wajao unataka utawaliwe vipi na wao. Je, kuna

mtu mwingine anayeweza kuwasilisha ipasavyo unachokitaka kiwe, matakwa yako,

matarajio yako maslahi yako na ndoto ya Tanzania uitakayo na ile ya wewe

mwenyewe unachotaka kuwa kama sio mwakilishi wako anayeguswa na

yanayokugusa?

Wewe kama mtumishi wa umma na ili mradi unatimiza wajibu wako huna sababu

kabisa ya wewe kuhusishwa na siasa kama hutaki. Vyama vinatakiwa vije

madarakani na kuondoka bila ya wewe kupoteza au kukosa chochote au kudhurika

kwa njia moja au nyingine, wewe na familia yako. Tazama kwa wenzetu

Ujerumani, Uingereza, Ufarsana na Mareknai mambo yanavyofanyika namna hii.

Mnakumbuka baadhi yenu mliokuwa wanafunzi wangu miaka ya kati ya muongo

huu na jinsi ambavyo Waziri Mkuu fulani alivyokuwa akiruhusu wawekezaji kuja

kwako moja kwa moja ili uwafanyie shotikati na jinsi wanavyotaka wao na sio

sheria na kanuni zinavyotaka na mkaja kunilalamikia, wengine mkilia kwamba

mmetukana ?

Hili ndio tatizo la kuwa na Katiba ambayo inaruhusu wapita njia, yaani, wanasiasa

wa vyama fulani kuathiri maisha ya watumishi wa kudumu mawizarani, mikoani na

wilayani. Serikali lazima iwe serikali kweli na haiwezekani na haikubaliki kabisa

kwa chama chochote cha kisiasa katika demokrasia ya kweli kuingilia kazi za

mtumshi wa umma.

No comments:

Post a Comment