JE, unajua wewe ndiye MMILIKI WA KATIBA na ndiye unayemwajiri rais, makamu wake, mawaziri na serikali nzima ?
Mzawa ana haki gani katika nchi yake. Na kwanini wazawa chini ya mzee wetu Iddi Simba wanakaa kimya wakati huu tunapotaka kuwa na katiba mpya ?
Maana, hakuna nchi iliyoendelea duniani ambayo imeendelea bila kutanguliza wazawa mbele iwe ni India, Malaysia, Norway, Finland, Denmark, Sweden, Indonesia, China, Korea na kadhalika. Tusijidanganye, maana kwa bahati mbaya pakitokea nuksi ya nyuklia kama ilivyotokea huko Japan au Chernobyl wageni pamoja na Watazania wasio wazawa wataondoka nchini mwetu na watakaobaki ni wazawa peke yao.
Hazina iliacha fedha BOT hadi zikaliwa na mafisadi. Katika nchi inayowajali wazawa wake fedha hizi zilihitaji kutumika katika kuwaamsha, kuwaelimisha na kuwaendeleza wazawa katika biashara mbalimbali, kilimo, viwanda vidogo na utoaji huduma ambao kwa umoja wake ugnelikwenda mbali sana katika kukuza GDP na Per capita ya Watanzania.
Tunapozungumzia usawa ni kosa kudhania eti watu weusi wa Tanzania tu ndio wazawa. Wapo wazawa Wahidni kama walivyo Waarabu na kina Mabala ambao ni Wazungu lakini ni Watanzania kuliko mtu mweusi eti.
Wala hatuwazii kabisa kumfukuza yeyote katika wao. Tunachotaka ni kuuona ule ukweli kuwa huwezi ukawafananisha hawa na Mkurya wa Nyamongo au Msukuma wa Geita ambaye ardhi yake serikali imetoa kwa wawekezaji na ikamuacha yeye patupu hana hili au lile. Mwarabu tajiri wa pwani mwenye ndugu zake Ughaibuni sio sawa na mzawa ambaaye hajawi kutoka kweny kijiji chake hapo Pwani kwa miaka yote hii huyu hahitaji kusaidiwa kwa kweli na asiposaidiwa na Benki Kuu na taasisi kama hizo ataondokana huyu na umaskini kweli, lazima tuwe wakweli jama. Maana uanasiasa wakati mwingine unatufanya kuwa wanafiki kupindukia. Unaweza kumuuza ndugu yako ili wewe upate tu cheo kwenye chama au serikali. Vibaya hivyo eti. Na Mola hapendi kabisa tabia kama hii ya unafiki na uzandiki na hasa dhidi ya wazawa wenzako ambao wewe leo umeneemeka, na wao kutokana na kuwa masikini unawaona eti ni ujinga na upumbavu wao ndio unaowafanya kuwa masikini.
Kwa wanaharakati kama mlivyona Haki Elimu, Haki Ardhi, Haki Mwanamke na kadhalika wakati umefika pia wa kuwa na Haki Mzawa ili kumnusuru masikini mkubwa kuliko wote Tanzania, mzawa wa nchi hii ambaye ni mtu mweusi bila haya wala aibu!!
No comments:
Post a Comment