MTANZANIA una haki ya wewe kuwa na mwakilishi katika chombo kitakachozungumzia na kisha kusaidia kazi ya kuandika katiba mpya. Katika wakati huu, wewe mwananchi, raia wa Tanzania unapanda cheo na kuwa ndiye mwajiri wa rais,makamu wa rais, mawaziri, wabunge na watumishi wote wa serikali. Kazi yangu katika mchakato huu ni kuwaambia viongozi hao kwamba: 'tunawataka mtutawale hivi na uwezo na sifa zenu ziwe hivi. Kinyume cha hivyo tutawafuta kazi..' endelea kurasa inayofuatia:
Friday, May 27, 2011
15. HAKIMU, JAJI
MAJAJI na MAHAKIMU mmeona hoja za Tundu Lissu zilizokuwa kwa yakini na
mashiko yote ya kisheria na haki kwa upande wenu yalivyopinduliwa katika
chombo kilichostahili kuwakilisha maslahi yenu. Kisha wakakubali eti wanasiasa
ndio wawe mabwana nidhamu wenu. Kwa mtaji huu hivi mnaamini kwamba kuna
mtu atakayewakilisha maslahi na kilio chenu cha miaka mingi kwa ukamilifu na
kuwatendea haki kama mwakilishi huyo siye mtu atakayetoka miongoni mwenu. Hii
sio sababu tosha ya nyie pia kudai kuwepo kwa Baraza la Katiba Mpya 2011 ?
Bila shaka Majaji, mahakimu na wanasheria wetu wameona 'laivu' jinsi ambavyo bunge letu linaweza kukabiliana na hoja za msingi zenye mantiki, ukweli na maana isiyokanushika wala kukatalika lakini bado bunge likakataa hoja hiyo au hoja hizo na kuamua tofauti na matarajio ya wengi.
Uweledi, ushujaa na uzalendo wa mbunge mpya na machachari Tundu Lissu ni ushahidi wa hili. Ingawa yeye ni mbunge aliamua kuona ukweli wa kuwa na mihimili ya kitaifa yenye nguvu na haki sawa bila upande mmoja kuudhulumu mwingine au kuunyima haki yake.
Ukweli huu haukuonekana na wabunge wa chama tawala ambao ghafla walipofuka macho na kushindwa kuona kutokana na uchama, umimi na ukabila wao wa kichama.
Hii ni nafasi yenu ya kipekee majaji, mahakimu na wanasheria au wanataaluma katika sheria kuona kuwa haki inatendeka siku zijazo kwa misaada ambayo nguvu ya hoja inaifanya istahili kushinda na sio kushindwa na hoja za mabavu, uchama na uwezo au maamuzi-kabla ya chama kinachotawala.
WATAKAOCHANGIA bila uchama, ukabila, ueneo, udini, ubinafsi na ushawishi wowote toka kundi lolote ndani au nje ya nchi watastahili kupewa tunzo ya juu kabisa ya Kitaifa.
NI haki na wajibu wenu pia kuwaamsha, kuwafundisha na kuwaelekeza wananchi wengine nini wanachopaswa kufanza ili mahitaji yao ya msingi, dhiki, mapungufu kwao, kasoro zilizopo kwenye maeneo na maisha yao, haki na maslahi yao yote yaweze kupatikana kwa kutumia katiba na sheria za nchi na sio vinginevyo.
Ni muhimu pia wananchi kuelewa kwamba serikali ni kitu kinachodumu milele mpaka mwisho wa dunia lakini vyama vya kisiasa ni taasisi za kupita, leo vinaweza kuwepo na kesho visiwepo na vikaja vyama vipya kabisa madarakani.
WATANZANIA tuna kila sababu ya kuikataa tabia inayojitokeza na kujijenga Afrika ya kuwatumia polisi na wanajeshi wetu kuwapiga, kuwatia ulemavu au hata kuwaua baba zao, mama zao, ndugu zao, kaka zao, dada zao, watoto wao, rafiki na jamaa zao. Na hili linataka demokrasia kamili, pana, refu na ya kina lakini wakati huo huo ikikataa usiri, uozo, uongo, ulaghai na kuwadanganya wananchi na rushwa, wizi na ufisadi unaolindwa na kuenziwa na chama cha kiasiasa ili kiendelee kubaki madarakani milele.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment