MTANZANIA wewe ndiye unayemwajiri rais, mawaziri, wabunge na watumishi wa
umma. Na wewe ndiye mmiliki wa Katiba. Na katiba ni mchakato wa wewe
kuwaambia watawala waliopo na wajao unataka utawaliwe vipi na wao. Je, kuna
mtu mwingine anayeweza kuwasilisha ipasavyo unachokitaka kiwe, matakwa yako,
matarajio yako maslahi yako na ndoto ya Tanzania uitakayo na ile ya wewe
mwenyewe unachotaka kuwa kama sio mwakilishi wako anayeguswa na
yanayokugusa?
TANZANIA ina kiola sababu ya kuwa muuza nyama, maziwa na asali mkubwa
Afrika ya Mashariki na Kati. Lakini hili linataka mipango mizuri, mikakati, sera na
utekelezaji unaowashirikisha wadau wote kwa kuunganisha masoko ya nje na
wazalishaji hapa nyumbani.
Kunahitajika ushirikiano na watafiti, washauri wa ujasirimali, uzalishaji mali,
menejimenti na masoko ili kifanyike kinachohitajika kufanyika kwa manufa ya
wafugaji wanyama, nyuki, mamba, ndege na hata nyoka kwa faida ya wafugaji hao
na taifa lao kiujumla.
No comments:
Post a Comment