Friday, May 27, 2011

31. MTOTO WA KIJIWENI.

NDUGU yangu unaona nuru au mwanga katika maisha yako. Nani anajua unavyoshinda na njaa; unavyotaka kuelimika lakini hakuna wa kukuelimisha; unavyotaka kuoa lakini uwezo huna; unavyotaka kuchukua nafasi yako katika kuchangia maendeleo ya nchi yako lakini hauna fursa.

Je, hivi kuna mtu anaweza kukuwakilisha wewe, mawazo na fikra zako na kadhalika ili viwemo ndani ya Katiba mpya. Kwanini usiwe na mwakilishi wako katika mkutano au baraza la katiba mpya?

Hvi upo hapo kijiweni kwa sababu ya kupenda au kwa kuwa umekosa mtu wa kuendeleza kipaji chako au kukusomesha au kukupatia ajira.

Unafikiri hawa wanasiasa wanaokupa samaki badala ya kukupa nyavu za kwenda kuvua wewe mwenyewe wanakusaidia?

Isingelikuwa vizuri uwepo wako hapa duniani uwe na sababu nawe uwe unaifuata sababu hiyo. Au inatosha tu kupewa ruksa na chama fulani kwamba hapa wekeni kijiwe chenu nasi tutawalinda. Na sio hawa hawa wanasiasa watakaowazuza hapo baadaye mwende pambana na vijana wenzenu toka vyama vingine mambo yatakapowaharibikia kama kilichotokea kwa Gbagbo na mwenzake Outtara ? Wao wako haki na wanafaidi maisha na walichokwiba na kupata kwa halali vijana wengi wameuawa, wamekuwa vilema na wengine wanateswa na kuozea kwenye magereza. Hii siyo njia ya kuchagua kwa kweli. Chagua kushiriki katika Baraza

la Katiba Mpya Tanzania ili uweze kufikisha unachotaka kuwa ili usije kutumika kama chakula cha risasi huko twendako.

No comments:

Post a Comment