JE, unajua wewe ndiye MMILIKI WA KATIBA na ndiye unayemwajiri rais, makamu wake, mawaziri na serikali nzima ?
Mkulima anauliza hivi:
i. Kilimo kwanza kitafanikiwa kwa sisi wenyewe kutengeneza Matrekta ya power-tiller yetu wenyewe au kwa kununua toka nchi za nje;
ii. Hatumo vitani je majeshi yetu yana mchango gan katika kufanikisha Kilimo kwanza angalau kwa kugeuza Nyumbu kuwa eneo la kutengeneza Power-tiller ya Kitanzania? Na kwanini jeshi na Meremeta (Mgodi wa dhahabu) wasidhamirie kuwa na jeshi linaljitosheleza kwa chakula na hifadhi zake mbalimbali.
iii. Hivi kuna mfumo na muundo wa shughuli za Kilimo cha Umwagiliaji Maji
unaoeleweka hapa nchini. Maana tunaamini kilimo cha umwagiliaji kikipangwa na kupangika kinaweeza kuondoa kabisa matatizo yetu madogo madogo ya chakula hapa nchini kwa miaka yote na hata kuwepo ziada ya kuuza nchi za nje;
iv. Nani wa kuwatafutia masoko ya ndani na nje ili nao pia kama kina Bakhressa au Azania au Mohammed Enterprise Limited waweze kuuza nje mazao yao maana linaokena hili halina tija kwa viongozi na wanasiasa?
v. Wakulima wakiwa na nyumba bora na safi, bustani zenye kunyweshwa kwa maji ya bomba, taa za umeme, mahala safi pa kula na pa kulala na vyoo bien, hivi Watalii toka ndani na nje ya nchi kama kijijini hapo patakuwa na vivutio viwili vitatu hawatapenda kweli kwenda kuwatembelea. Na hili halistahili kupotezewa muda kama tulivyopotezewa muda kwenye mengi mengine.
No comments:
Post a Comment