MTANZANIA wewe ndiye unayemwajiri rais, mawaziri, wabunge na watumishi wa
umma. Na wewe ndiye mmiliki wa Katiba. Na katiba ni mchakato wa wewe
kuwaambia watawala waliopo na wajao unataka utawaliwe vipi na wao. Je, kuna
mtu mwingine anayeweza kuwasilisha ipasavyo unachokitaka kiwe, matakwa yako,
matarajio yako maslahi yako na ndoto ya Tanzania uitakayo na ile ya wewe
mwenyewe unachotaka kuwa kama sio mwakilishi wako anayeguswa na
yanayokugusa?
Dereva na konda mnatukanwa na wenye mabasi, hamna ajira, mnatukanwa na
trafiki na wanafunzi na mnadhulumiwa na wenye vituo vya mafuta na kadhalika.
Yote haya ni mambo ambayo kama nchi ingelikuwa na sera, taratibu na kanuni
sahihi za uendeshaji mambo yasingewapa shida kwa kiasi cha shida mnazopata
leo. Mna kila haki ya kuwasilisha maoni yenu hadi ngazi ya juu kabisa ya tamko la
taifa kuipitia mchango wenu kwenye Baraza la Katiba Mpya 2011.
Udereva sio kazi ndogo. Ungelikuwa kazi ndogo pasingekuwa na madereva
wanaolipwa 250,000/-500,000- kwa mwezi kwa kuendesha wakubwa. Au hamjui?
Mna kila sababu ya kudai ajira za kudumu, kutetea maslahi na marupurupu yenu
na usalama wenu kazini na wakati ni huu kuotkana na fursa inayoletwa na
mchakato wa Katiba mpya nchini. Ila ni lazima muwe na mwakilishi wenu msije
kuwakilishwa na waajiri wenu!
No comments:
Post a Comment