UNGELIPENDA kuwa na nchi ya aina gani unapokuja kuwa mtu mzima. Je, kuna mtu yeyote anayeweza kukusemea fikra, ndoto, maoni, matarajio na matazamio yako. Unahitaji uwakilishi wa vijana wenzako au wazee na wasomi waliosahau ujana na maisha ya kijana na hofu na
matarajio yake yakoje?
Asilimia hamsini au zaidi ya Watanzania leo ama ni watoto au vijana. Na idadi hiyo inazidikukua siku hadi siku. Katika maendeleo ya nchi yoyote duniani wakati hufika ambapo idadi ya vijana huwa kubwa zaidi kuliko watoto au wazee katika nchi. Kwa kuwa vijana ndio wenye akili angavu zaidi na uwezo zaidi kiaakili na kifikra huu huwa ni wakati muhimu wa kujenga nchi na kuitoa kwenye ngazi ya chini na kuipeleka ya juu au za juu zaidi. Lakini hili hutegemea ni aina
gani ya uongozi uliopo madarakani.
Uongozi ukiwa ni ule wa kuwadanganya wananchi wa samaki wa kila siku badala ya kuwawezesha vijana kwenda kuvua wao wenyewe huishia kuingia kwenye matatizo.
Yanayotokea Misri na nchi za Maghreb na kwingineko Uarabuni ni nchi kuwa na vijana wengi lakini ikashindwa kuwashughulisha vijana hao.Na kama biblia inavyosema nadhani katika Mitahali, mikono isiyokuwa na kazi ya maana ya kufanya basi shetani huwa hachelewi kuitumia.
Je, ni nani atakayewanusuru vijana wa nchi hii na majaliwa hayo kama sio wao wenyewe au wawakilishi wao katika Baraza la Katiba la Kitaifa Tanzania 2011 ?
No comments:
Post a Comment