WATANZANIA walioko nchi za nje wana mitihani mingi na wakati mwingine hunyimwa haki zao za msingi ikiwemo kupiga na kupigiwa kura.
Je, mwenzangu uliye Ughaibuni unadhani una haki ya kupiga kura hata kama hauishi nchini. Utafanya nini ili upate haki hii . Ni nani atakaykupigania haki yako.
Na katika nchi kubwa kama vile Marekani, Uingereza, Urussi, Japani, Uchina, Ujerumani, India, Indonesia, Malaysia na nyinginezo kwanini nchi yetu isiwe na majengo, mahoteli na mahosteli kwa ajili ya kuwawezesha Watanzania wanaokwenda huko kimasomo au kujifunza kitu fulani, kwa tiba, kazi, biashara, utalii na kadhalika kukaa kwa gharama za chini na katika mazingira wanayofurahia kuwaona, kuzungumza na kukaa na Watanzania wenzao pamoja na kuwemo katika nchi ya nje?
Sehemu hizo kwa kuwa zitaendeshwa nusu-kibiashara zitakuwa zikijiendesha zenyewe kwa ruzuku ndogo sana toka serikali na ufadhili wa Watanzania ambao watakuwa wamenufaika na kuneemeka kutokana na kupitia kwenye sehemu kama hizo kabla hawajaukata.
No comments:
Post a Comment