MTANZANIA wewe ndiye unayemwajiri rais, mawaziri, wabunge na watumishi wa umma. Na wewe ndiye mmiliki wa Katiba. Na katiba ni mchakato wa wewe kuwaambia watawala waliopo na wajao unataka utawaliwe vipi na wao. Je, kuna mtu mwingine anayeweza kuwasilisha ipasavyo unachokitaka kiwe, matakwa yako, matarajio yako maslahi yako na ndoto ya Tanzania uitakayo na ile ya wewe mwenyewe unachotaka kuwa kama sio mwakilishi wako anayeguswa na yanayokugusa?
Ni lazima mkopeshaji naye alindwe na kupata haki zake. Lakini hilo linakuwa rahisi kama mkopeshaji huyo anawatendea haki wale anaowakaposha, yaani, wakopaji.
Kukopa na kukopesha ni kitu kizuri katika jamii kama kinafanya kazi iliyokusudiwa nayo si ya kamari bali ya kinyenzo kama msaada unaokuja usipotegemewa kumuondoa mtu katika hali duni na dhaifu na kumpeleka katika hali bora. Ikiwa ni kinyume cha hivyo basi huitwa mtego na umumiani wa kiuchumi ambao unakuwa hauna faida kwa mwananchi.
Mkopeshaji lazima afikirie sikuzote kuwa tofauti na wenzake na katika kuwa tofauti huku ni lazima Benki Kuu na serikali vimzawadiwe kwa njia moja au nyingine. Kwa mfano, kuzuka kwa benki ambazo wafanyakazi wengi watakuwa mitaani kukutana na watu mbalimbali wakiwemo wazalishaji mali, wakulima, wafanyabiashara na wajasiriamli wengine kwa nia ya kuwashauri na kuwaendeleza katika shughuli zao kama Benki za Wajapani zinavyofanya kuanzia mwaka 1955 itakuwa na uwezo wa kufanya maajabu kuliko benki nyingine nchini.
Na hili haliwezekani bila wakopeshaji wenyewe kuwa na ubia na wakopaji katika shughuli zao kwa faida ya pande zote.
No comments:
Post a Comment