MTANZANIA wewe ndiye unayemwajiri rais, mawaziri, wabunge na watumishi wa
umma. Na wewe ndiye mmiliki wa Katiba. Na katiba ni mchakato wa wewe
kuwaambia watawala waliopo na wajao unataka utawaliwe vipi na wao. Je, kuna
mtu mwingine anayeweza kuwasilisha ipasavyo unachokitaka kiwe, matakwa yako,
matarajio yako maslahi yako na ndoto ya Tanzania uitakayo na ile ya wewe
mwenyewe unachotaka kuwa kama sio mwakilishi wako anayeguswa na
yanayokugusa?
Inavyoelekea hivi leo Benki, Vyama vya Kuweka na Kukopa, taasisi za
Microfinacne na wakopeshaji wa aina zote wananufaika zaidi ya Mtanzania
anavyonufaika na kuna madai ya taasisi hizo kuwanyonya watu.
Je, ili sisi kama wakopaji wa Kitanzania tunahitaji Taasisi gani za fedha ? Na nini
iwe mchango wa Benki Kuu, NSSF, PPF, LAPF, NHSF na wengine kama hao?
Na, je, makampuni ya simu ambayo sasa yanatukopesha kisirisiri na kucheza
kamari zinazotula kila siku hazivuni kupita kiasi. Je, mashirika kama haya ya simu
hayastahili kuwekea sheria ya kuuza sehemu zao za hisa kwa wananchi ili
kugawana na Watanzania mabilioni yote wanayoyafaidi kila mwezi ?
No comments:
Post a Comment