Thursday, May 26, 2011

NINAKAMILISHA KAZI NILIYOIANZA 1990...

Toka ukurasa wa mbele:


Katiba si mali ya chama fulani cha siasa na wala siyo mali ya serikali na wala siyo mali ya rais. Mwenye kumiliki katiba ni wewe Mtanzania, mimi na yule kwa umoja wetu.

Ninashukuru Mungu kuniwezesha kuendelea na kuhitimisha kazi hii niliyojipa mwenyewe ya kuona kwamba Tanzania inakuwa ni nchi na taifa la kuigwa katika demokrasia, haki za binadamu, uwajibikaji kwa wananchi wake na sio tu katika suala la amani, umoja na mshikamano wa kulazimisha kwa kutumia vyombo vya dola.
Nilianza na Blogi ya Demokrasia Tanzania na Afrika na ninamalizia kazi hii kwa blogi ya 4 - BARAZA LA KATIBA MPYA TANZANIA 2011. Allahamdulillahi na Inshallah Watanzania watapata kilicho bora, safi na kisicho na kasoro kwa faida ya vizazi vijavyo.

Baraza la Katiba la Taifa au Mkutano wa Kitaifa wa Katiba unastahili kushirikisha makundi yote ya kikazi, kishughuli, kimaeneo na kimaslahi bila kukosekana mwakilishi hata mmoja. Na hoja zetu ni kama zinavyoainishwa katika nafasi za uwakilishi tarajiwa kama ilivyo katika blogi hii:

No comments:

Post a Comment