Friday, May 27, 2011

16. MWANASIASA, MBUNGE.

WANASIASA wote mnastahili kuwa na mwakilishi kutoka chama chenu kwenye

Baraza au Mkutano wa Kitaifa wa Katiba Mpya 2011 na sio vinginevyo. Maana nyie

ndio vinara wenyewe na washughulikia siasa wakuu na wasimamizi wakuu

baadaye wa haki za raia wote.

Kila chama kina mipango, mikakati,sera na mbinu za kuendeleza jamii ya

Kitanzania. Mathalani, kuna wanaopinga kuwepo kwa serikali huru za mikoa kwa

madai kwamba kufanya hivyo kutavunja umoja na amani yetu. Wakati wengine

wanaunga mikono mikoa kuwa na waziri mkuu wake, mawaziri wa mkoa na

wawakilishi wa mkoa kama vile ile inayoittwa nchi ambayo ni ndogo kwa eneo na

idadi ya watu kuliko mikoa mingi Tanzania ilivyo iitwayo Zanzibar.

Isitoshe wanasiasa wanatofautiana katika masuala ya Muungano, mbinu bora za

kubinafsisha au kutaifisha tena mashirika, viwanda na vyote vilivyoshindwa

kufanya kazi hadi wa leo, Haki za binadamu, elimu bure au elimu kulipiwa na

wazazi au walezi, mikakati sahihi ya kuipatia nchi maji dhidi ya mikakati mibovu,

uhuru wa mtu na uhuru wa vyama na vikundi vya watu,Uwekezaji, uzawa,

Uchimbaji madini na mrabaha, kasi ya kuleta demokraasia,nafasi ya mabenki na

taasisi za fedha katika jamii, kuwepo au kutokuwepo mashirika au makampuni ya

umma, umilikaji na uendeshwaji wa vyombo vya habari vya serikali na kadhalika.

Yote haya yanahitaji mawazo tofauti na mchakato

Kuwepo kwao katika Baraza la Katiba Mpya Tanzania 2011 kutachangia sio haba

kupata katiba bora zaidi na mwelekeo mpya wa kisera, kimpango na kimkakati

katika miaka ijayo ili kuwa na Tanzania madhubuti, bora, safi na tajri kuliko hii ya

sasa. Inshallah!


WATAKAOCHANGIA bila uchama, ukabila, ueneo, udini, ubinafsi na ushawishi wowote toka kundi lolote ndani au nje ya nchi watastahili kupewa tunzo ya juu kabisa ya Kitaifa.

NI haki na wajibu wenu pia kuwaamsha, kuwafundisha na kuwaelekeza wananchi wengine nini wanachopaswa kufanza ili mahitaji yao ya msingi, dhiki, mapungufu kwao, kasoro zilizopo kwenye maeneo na maisha yao, haki na maslahi yao yote yaweze kupatikana kwa kutumia katiba na sheria za nchi na sio vinginevyo.

Ni muhimu pia wananchi kuelewa kwamba serikali ni kitu kinachodumu milele mpaka mwisho wa dunia lakini vyama vya kisiasa ni taasisi za kupita, leo vinaweza kuwepo na kesho visiwepo na vikaja vyama vipya kabisa madarakani.

WATANZANIA tuna kila sababu ya kuikataa tabia inayojitokeza na kujijenga Afrika ya kuwatumia polisi na wanajeshi wetu kuwapiga, kuwatia ulemavu au hata kuwaua baba zao, mama zao, ndugu zao, kaka zao, dada zao, watoto wao, rafiki na jamaa zao. Na hili linataka demokrasia kamili, pana, refu na ya kina lakini wakati huo huo ikikataa usiri, uozo, uongo, ulaghai na kuwadanganya wananchi na rushwa, wizi na ufisadi unaolindwa na kuenziwa na chama cha kiasiasa ili kiendelee kubaki madarakani milele.

No comments:

Post a Comment