Friday, May 27, 2011

38. MFANYABIASHARA.

JE, unajua wewe ndiye MMILIKI WA KATIBA na ndiye unayemwajiri rais, makamu wake, mawaziri na serikali nzima ?

Wafanyabiashara wana malalamiko yao mengi kuhusiana na nishati ya umeme, kodi kubwa za serikali za mitaa na serikali kuu, sera na kanuni mbovu za kibiashara, kubebeshwa mizigo isiyokuwa yao; mazingira duni ya nchi; kipato kidogo cha wananchi; matumizi madogo ya teknolojia na kadhalika.

Wao, hata hivyo, bado wanaamini kwamba Tanzania inaweza ikawa kitovu cha biashara kwa Afrika Mashariki, Kati na Kusini ili mradi serikali ijipange kuwathamini na kuwategemea wafanyabiashara wa ndani kuliko wale wa nje kama ilivyo hivi sasa.

Wanasema hapana sababu ya Wakongomani, Wazambia, Wamalawi, Waburundi,

Wazimbabwe, Warwanda, Waganda na Wasudani kwenda kununua vitu toka China na Dubai, Imarati.

Serikali yenye serikali huru kiuchumi na kijamii za mikoa pembezoni mwa nchi zinaweza kabisa kugeuza mikoa hiyo kuwa ni Dubai na Hong Kong za Afrika. kInachohitajika ni kufunga masikio na mcho kwa viongzi wetu na kisha kuwapa sapoti wafanyabiashara kwa kuwa na ndege na meli za Kibiashara zinazoendeshwa kwa tija, ufanisi na ufanifu wa hali ya juu.. Na kisha kuwa na vituo vya mipakani ambavyo ubora na uzuri wake utakuwa kama ule wa viwanja

vya ndege vya Dubai sio vya sasa hivi vya Tanzania. Mengine watamalizia wafanyabiashara wao wenyewe. Na fumba na kufumbua mikoa iliyokuwa nyuma kiuchumi kama Kagera, Kigoma, Tabora, Ruvuma, Rukwa, Mtwara itafanya maajabu ya kiuchumi.

No comments:

Post a Comment