Friday, May 27, 2011

9. OFISA MISITU

WEWE ofisa misitu wilayani Kisarawe ambaye serikali toka ikupeleke huko

imekusahau kabisa na ofisi yenu ina fenicha za mwaka 1940 na kijumba chenyewe

kinatishia kusambaratika wakati wowote hivi unadhani kweli usipowakilishwa na

wewe mwyewe au mtu anayefanya kazi kama yako mawazo na mchango wa

kuboresha maisha yako leo na kesho itapatikana na itatendewa haki katika

mchakato wa Katiba mpya.


Haiwezekani. Amka. Zinduka na dai haki yako ya kuwa

na Mwakilishi wako katika Baraza au Mkutano wa Kitaifa wa Katiba Mpya na

usikubali kabisa kuwakilishwa na wasiojua wapi kunguni na chawa

wanaokusumbua walipo.


Kwa upande mwingine ni wajibu wa wakuu wako wa kazi kama kweli wanataka

kuhakikisha kwamba wewe si mwizi wa mali asili ya nchi hii na haushirikiani na

majangili na wavunaji misitu isivyo halali ni lazima wahakikishe unapewa fursa ya

kuwakilishwa ili uifanye kazi yako kizalendo nawe upate mahitaji yako ya msingi na

ziada kutokana na kazi yako bila kuvunja sheria

za nchi.


HakiKatiba: Mchango wa Mabwana na mabibi Misitu ni Muhimu sana. Nao wawepo kwenye Baraza la Katiba Mpya 2011 ili wizi na uharamia kwa misitu na mali asili ya nchi hii vikome!

No comments:

Post a Comment