Friday, May 27, 2011

20. BAHARIA NA MARUBANI

NCHI YETU imepoteza ajira nyingi kwa mabaharia, wafanyakazi wa relwe na

wafanyakazi katika ndege na viwanja vya ndege kutokana na viongozi wetu

kushindwa kuhakikisha kuwa mashirika husika yanaendeshwa kwa ufanisi na

ufanifu.

Je, kuna yeyote yule atakayewasilisha mawazo, fikra, imani na matarajio yenu

kuhusu vyombo hivi ila nyie wenyewe au wawakilishi wenu katika mkutano au

baraza la kuandika katiba mpya?

Tukiacha ujinga na upumbavu wa kujitanya tunajua kila kitu na kuwachagua

mameneja wa mashirika nyeti kama wale wa mashirika ya ndege, relwe, meli na

vyombo vingine vya usafiri na tukautanguliza Utanzaznia badala ya ujuzi, uzoefu,

utaalamu na uwezo wa mtu kuongoza iwe Mtanzania au isiwe Mtanzania hatutafika

mbali.

Haya mambo ya nchi nzima kutawaliwa na wafuasi wa chama kimoja tu ndiyo

yametufikisha hapa tulipo leo. Maana ni wanachama hao hao waliokuwa pia

wasimamizi wa mashirika mengi yaliyokufa.

Isitoshe Watanzania wengi wenye uwezo, akili, busara, hekima, ujuzi ulio na soko

na vipaji maalum sio wote wako kwenye chama tawala. Kusimamia uchumi sio

sawa na kusimamia siasa. Katika kusimamia uchumi ni lazima tuachane kabisa ya

kuchagua viongozi kwa sababu ni wananchama na sio kwa sababu wana uwezo

wa kuendesha kitu fulani.

Hasara tunayoipata ndiyo hii ya nchi yetu kukosa shirika la ndege kwa kuwa

mamaneja walikuwa wanachama wa chama fulani. Na mashirika ya relwe ndioi

kama vile hayapo na huko kwenye bahari na kwenye maziwa Tanzania na

Watanzania hawana hata chombo kimoja cha maana cha kujivunia kama watu na

nchi.

Wewe nahodha, baharia au mfanyakazi melini au kwenye ndege unaamini hivi

kweli kuna mtu anayeweza kuwakilisha kilio chako na matarajio yako isipokuwa

mwakailishi wako ambaye atayachukua na kuyapeleka kwenye Baraza la Katiba

Mpya Tanzania 2011 yote yaliyo akilini mwako ili yasikilizwe na kuzingatiwaa

katika kuandika Katiba Mpya ?

No comments:

Post a Comment