Ewe mwanamke wa Kitanzania ungelipenda kuendelea kuwa mpiga vigelegele, mhudumu na mshangiliaji na mpigaji makofi kwa wanaume au unadhani wakati wa mabadiliko umefika. Hebu jiulize maswali haya:
i. Nini kifanyike ili yanayotokea Uarabuni,Sudan, Kongo na Burundi yasitokee Tanzania ?
ii. Hivi mnastahili kuwa na UMOJA WA WANAWAKE WA TANZANIA (TANZANIA) au Umoja wa Wanawake Tanzania (CCM) ?
iii. Hivi kweli mnahitaji viti na vyeo vya kupewa au mnahitaji mipango na mikakati ya kutumia akili, nguvu na uwezo wenu wenyewe kujiendeleza?
iv. Tuwaangalie vipi wagonjwa wanawake na wajane nchini mwetu?
v. Tumkomboe vipi mwanamke wa vijijini?
vi. Tumewezeshe vipi mwanamke wa Kitanzania ili asibebwe bebwe kila saa?
vii. Tumpe vipi mwanamke wa Kitanzania Uhuru wa kuabudu kwa mujibu wa dini yake ikiwemo pia kuwa na Mahakama ya Kadhi kwa faida ya Wanawake wa Kiislamu na jamaa/jamii yao?
viii. Wanawake wanawezaje kuishinikiza serikali na wanasiasa ili nchi iwe na demokrasia ya kweli na uheshimuji haki za binadamu kwa mapana na marefu? Tukizingatia kwamba wanaoteseka na kuaibika kunapokoseakana demokrasia ya kweli zaidi ni wanawake?
No comments:
Post a Comment