Friday, May 27, 2011

4. NESI.

MANESI wetu wanalaumiwa hivi leo kwa kila jambo lakini ukangalia kwa undani ni

suala la mishahara tu na maslahi.



Kwa mtu anayefanya kazi wakati mwingine masaa 10 au zaidi kwa siku,

anayekosa usingizi mara kwa mara na anayetakiwa kutoa huduma ambazo wengi

wetu tutafikiri mara mbili kukubali kuzifanya wakati umefika kwa kweli kuangalia

uwezekano wa kuwa na kima cha chini cha mshahara ambacho kitawavutia

wanawake na wanaume wenye wito kufanya kazi hii ya unesi kwa huruma,

mapenzi na uvumilivu.


Je, wewe nesi unadhani kuna mtu anaweza kuwakilisha kilio, mahitaji, matakwa na

matarajioa yako ila nesi mwenzako uliyemchagua kwenda kusema unachokittaka

kiwekwe hadharani?


Zingatia kuwa serikali na wananchi wa Tanzania wana uwezo wa kuzifanya

hospitali zetu kuwa bora kiasi ambacho wagonjwa wengi katika nchi mbalimbali za

Kiafrika wakaja hapa kutibiwa na kuuguzwa badala ya kupelekwa nchi za nje ? Na

hili likifanyika ni kwamba mishahara, marupurupu yenu na kipato chenu kwa

ujumla kitaongezeka na hamtakuwa na sababu ya kukimbilia nchi za nje !



Jitayarisheni, jiandaeni na kujihami na nguvu za hoja kuhusu umuhimu wa kuwa

na Baraza au Mkutano wa Kitaifa wa Katiba Mpya 2011 na wala sio Tume au

Kikundi cha wateuliwa wachache hata kama ni mawaziri, wabunge, majaji,

wanasheria na engineo kama hao, maana historia inaonesha wote hao hawawezi

kutetea maslahi yako wewe na kwamba mwamba ngoma ngozi lazima avutie

kwake au sio?



NCHI inayowaheshimu madaktari na manesi wake na kuwa na mazingira mazuri kwa wafanyakazi na wagonjwa mahospitalini inaweza kupata fedha za kigeni kutokana na kuja kwa wagonjwa wengi kutoka nchi jirani na za mbali kutibiwa hapa kwetu.



HakiKatiba 2011:
Hospitali zetu zikiwa nzuri, daktari na manesi wetu wakaridhika tunaweza kupata mabilioni ya fedha za kigeni!

No comments:

Post a Comment