WANAKIJJI ni watu waliosahaulika sana. Kilichoonekana muhimu kwao na
pengine wamekipata hadi wa leo lakini kwa baadhiya wanavijiji tu ni zahanati,
shule na matawi ya vyama vya siasa vilivyo hoi bin taabani.
Upo umuhimu wa Hazina kuchangia kuwa na matawi imara na madhubuti ya
vyama vyote vya siasa katika kila kijiji na mipango ikafanyika ya kuwawezesha
viongozi wote wa vyama vya kisiasa kuajiriwa kwa njia moja au nyingine na
kulipwa na vyama vyao kutokana na mapato yao na misaada toka Hazina na
wafadhili wanaosaidia harakati halali za kidemokrasia zisizo na nia ya kuichafua
nchi.
Kodi ya wananchi inapotumika kuviendesha vyama vya siasa sio kitu kibaya kwa
maana ufadhili wa nje ni hatari zaidi. Na fedha hizi ni MTAJI WA KIJAMII halisi
ambao unaweza ukawa na thamani kubwa kuliko hata mtaji wa kifedha katika
maendeleo yetu.
Demokrasia na haki za binadamu zikishashamiri vijijini itakuwa ni rahsi wanavijiji
sasa kudai maji ya bomba wakapata; kudai umeme wakapata; kudai barabara safi
na ikawepo; kutafuta masoko ya mazao yao ndani na nje na wao wenyewe
wakauza wanacholima na kuvuna bila kupitia mkononi mwa walanguzi na wakorofi
wengine.
Ni kwa namna hii huduma zilizopo kama vile zahanati, shule, ujenzi wa nyumba za
kisasa vijijini, maoko, bustani za kupumzika, viwanja vya michezo, mawasiliano,
usafi na utunzaji mazingira navyo vitaboreshwa na kusasaishwa zaidi.
WANAVIJIJI walio na uchungu na maendeleo ya vijiji vyao ndio wanaotakiwa
kuleta katika Baraza au mkutano wa katiba mpya ruia na matarajio haya ili
yafaniwe kazi katika katiba na iwe ni kosa kukubali wanavijiji kukosa maji, umeme,
barabara na huduma zingine za msingi na za ngazi ya juu zinazohitajiwa nao.
No comments:
Post a Comment