Friday, May 27, 2011

41. MFUNGWA.

JE, unajua wewe ndiye MMILIKI WA KATIBA na ndiye unayemwajiri rais, makamu wake, mawaziri na serikali nzima ?

Wazungumzaji wetu wa jana na juzi kuhusu wazawa na wakereketwa wengine wazawa hii ni nafasi yenu ya nyie kujumuika katika Baraza au Mkutano wa Katiba Mpya 2011 kuzungumzia jinsi Katiba mpya itakavyowasaidia kuwa na 'level field' na 'startup seeds' ili muweze ku-catch up na wale ambao tayari wana mali na mitaji ya kwuafanya wao kuendelea kuwa matajiri na matajiri zaidi kwa kutunyonya sisi tusio na kitu.

Na je, unajua kwa Kuwa mfungwa katiba haistahili kukunyima haki yako ya kuishi kama binadamu na sio mnyama?

Historia ya wafungwa na magereza huko Ulaya na hususan toka kwa Mwingereza ilikuwa ya kumgeuza raia wao kifungoni kuwa ni 'mnyama' asiyestahili haki yoyote. Tulipodai na kupata uhuru toka kwao tulirithi mengi mabaya tukaacha yale yaliyokuwa mazuri.

Moja kati ya yale tuliyoyarithi ni hili la kumgeuza mnyama mfungwa na sio tena binadamu. Kwetu imefikia kuanza hili hata tu mtu anapokuwa mahabusu na hajahukumiwa na kukutwa na kosa.

Mfungwa una haki ya kuuliza umekosa nini kwa wanasiasa wetu kiasi cha wewe kugeuzwa mnyama tena mnyama hatari sana ?

Matokeo ya hili nenda kwenye jela za Marekani na Uingereza zimezua unyama na ubaya zaidi kati ya wafungwa. Kwa sababu ukishamgeuza mtu kuwa mnyama na kweli anageuka kuwa mnyama. Je, yanayotokea Uingereza ndiyo tuanayotaka yatokee hapa Afrika?

Twendeni kuliko na magereza ya kistaarabu na kujifunza yaliyo bora na sio kugeuza magereza yetu kuwa 'Sodom na Gomorrah' hapa Afrika kwa sababu tu, tunawanyima wanaume haki ya kukutana na wake zao! Na kisha wanaume wao kwa wao wanageuza mabibi na mabwana. Kiasi kwamba kuna mapolisi na maofisa magereza wanaoshabikia hili.

Tunashindwa kutambua kwamba kuna siku ya siku kama tutaendelea hivi sisi wenyewe viongozi na polisi kama ilivyotokea Misri tunaweza kuwa naio wafungwa na wale tuliokuwa tukiwatesa ndio viongozi na mapolisi.

Kuyageuza magereza yawe ya kistaarabu ni kwa faida yetu sote, na hili kwa hakika lina mengi mazuri ikiwa ni pamoja na kumuogopa Mwenyezi Mungu na kupata baraka na rehema zake katika maongozi ya nchi na watu wake.

Magereza yetu kama ndoto ya baadhi ya waasisi wa nchi hii yanaweza yakawa darasa kma sio shule kubwa tu ya kumbadili binadamu mwovu kuwa mtu mwena kuliko wote. Na hili haliwezekani kwa kumgeuza mfungwa mnyama huko gerezani. Bali kwa kumuonesha utu na ubinadamu wa hali ya juu.

No comments:

Post a Comment