Thursday, May 26, 2011

45.. MWANAHARAKATI.

MWANAHARAKATI uwe umetoka TAMWA, MISA, LHRT na kwingineko hii utalazimika kuweka kando shughuli nyingine zote ili wewe uwezeshe makundi mengine yote hapo juu na hapa chini yaweze kufanikisha azma ya Watanganyika na Wazanzibari chini ya Utanzania wao kuwa na Katiba itakaytotoa haki kwa pande zote mbili za nchi kwa kuzingatia mambo zaidi ya yanaozingatiwa hivi sasa. Ijulikane pia mikoa mingi inauliza hivi Zanzibar yenye wapiga kura laki nne (400,000) sawa na wapiga kura wa jimbo la Ubungo, Dar es salaam, Tanzania bara kuwa na rais, waziri mkuu wake na bunge lake hivi tunaifanyia haki mikoa ya Tanzania bara. Kwanini Arusha, Kagera, Mwanza, Tabora na mikoa yote iliyobakia nayo isiwe na serikali yao kama Zanzibar ilivyo kwani mikoa hiyo imewazidi Zanzibar kwa ukubwa wa eneo na idadi ya watu. Mikoa itakayokuwa pia na serikali huru kiuchumi na kimkoa chini ya Waziri Mkuu wa Mkoa, Mawaziri wa Mkoa na Bunge la Mkoa husika?

Kuna wanaodai eti Mkoa wa Mara ungelikuwa na Waziri Mkuu wake, Mawaziri wake akiwemo wa Madini na bunge lake yale yaliyotokea huko hivi karibuni yasingelitokea maana serikali hiyo ingekuwa daima inawalinda kwanza wakazi wake na sio watu wengine!!

No comments:

Post a Comment