WEWE mkazi wa mkoa fulani hivi unadhani mkoa wako utaendelezwa kwa
kutegemea viongozi, rais, mawaziri,wabunge na watumishi wa umma wanaoishi na
kula upepo wa bahari ya Hindi jijini Dar es salaam au unahitaji sana serikali
iliyokuwa karibu na wewe katika kufanikisha maendeleo yote ya mkoa ikiwemo
yale ya kiuchumi, kijamii, kisiasa, kiutamaduni, kimichezo, kiteknolojia na kimaisha
kwa ujumla.
Mimi ninaamini ewe Mtanzania mwenzangu uliyeko Arusha, Mwanza, Mara,
Mbeya, Kilimanjaro, Ruvuma, Kagera na mikoa iliyosalia kwamba wakati umefika
wa kuondokana na viongozi wanaotembelea mikoa yetu mara moja kwa mwaka
kama sio kila baada ya miaka 5 kunpokuwa na uchaguzi. Na tunahitaji viongozi
ambao ukiamka asubuhi unaweza kusema leo naenda kwa Waziri Mkuu au waziri
wangu kwenda kumwambia anifanyie hiki maana huyu ni mtumishi wangu, mimi ni
mwajiri na yeye ni mfanykazi wangu. Kinyume cha unavyokwenda kwa Mkuu wa
Mkoa au Mkuu wa Wilaya ukitetemeka na ukiamini kwamba yeye ni Bwana
Mkubwa, Tajiri, Bosi wako wakati mambo yanatakiwa yawe kinyume cha hivyo.
Njia ya kufanikisha hili, ndugu yangu Mtanzania, ni kuendelea kuwa na serikali ya
Muungano wa Tanzania na Mikoa yetu ambayo mingi ni mikubwa kieneo na kwa
idadi ya watu kuliko Zanzibar yenye watu milioni moja tu -kuwa na Serikali huru
kiuchumi na kijami za mkoa.
Serikali ya Mkoa itakuwa chini ya Waziri Mkuu wa MKoa (kama ilivyo Ujerumani au
India); chini ya Waziri Mkuu kutakuwa na Baraza la Mawaziri wa Mkoa
watakaotokana na wawakilishi wa wananchi watakaochaguliwa kutoka maeneo
mbalimbali lakini pia watakaotokana na makundi ya kimaslahi katika mkoa husika.
Tofauti na serikali kuu mawaziri wa mkoa watakaotokana na ubunge
wakishachagulwa kuwa mawaziri wataachia nafasi zao za ubunge kwa watu
wengine, ili wabunge wafanye kazi moja tu nayo ni ya kuwakilisha wakazi wa
maeneo au makundi maslahi yao.
Hii ina maana CHADEMA au CUF au NCCR huko tunakokwenda inaweza ikawa
na Waziri Mkuu wa Mkoa na wawakilishi/wabunge wengi kutoka chama hicho na
hivyo kuunda srikali yao. Kwa maneno mengine, CCM inaweza ikawa imeshika
uongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini mkoa wa Kilimanjaro au
Mara ukawa chini ya serikali ya CHADEMA na hivyo kuleta chachu kali na
ushindani mkali wa kuuendeleza mkoa na watu wake kuliko nchi nzima inapokuwa
chini ya chama kimoja tu cha kisiasa.
Hili hakika ni jambo zuri na la kupigiwa debe. Na ni wewe mkazi wa mkoa husika
unayeweza kuleta mapinduzi haya makubwa ya kimuundo na kimfumo wa serikali,
jambo litakalochangia kuwepo kikweli kweli kwa ari, kasi na nguvu mpya katika
mandeleo ya nchi na mikoa yake shirikishi kuliko ilivyokuwa huko nyuma.
No comments:
Post a Comment