MTANZANIA wewe ndiye unayemwajiri rais, mawaziri, wabunge na watumishi wa
umma. Na wewe ndiye mmiliki wa Katiba. Na katiba ni mchakato wa wewe
kuwaambia watawala waliopo na wajao unataka utawaliwe vipi na wao. Je, kuna
mtu mwingine anayeweza kuwasilisha ipasavyo unachokitaka kiwe, matakwa yako,
matarajio yako maslahi yako na ndoto ya Tanzania uitakayo na ile ya wewe
mwenyewe unachotaka kuwa kama sio mwakilishi wako anayeguswa na
yanayokugusa?
Wakubwa wamekutekeleza, wamekupuuza, wamekudharau na wamekusahau kwa
miaka yote hii na sasa wao wenyewe ndio wanaojifanya wataalamu zaidi yenu
katika masuala ya kilimo na kufanya maamuzi juu ya vichwa vyenu. Je, unadhani
kilio chako na matarajio yako yatafikishwa na nani kama pasipokuwepo na Baraza
au Mkutano wa Kitaifa wa Katiba Mpya 2011 ?
11. MENEJA, MKURUGENZI MTANZANA
RAIS wenu mmoja toka chama tawala aliwatoa manani kabisa na kusema
hamuwezi chochote na wala siyo nyie mtakaoijenga Tanzania bali wawekezaji na
mameneja kutoka nje.
Huu ni wakati muafaka wa kutokosa nafasi yenu ya uwakilishi katika Baraza au
Mkutano wa Kitaifa wa Katiba Mpya 2011 ili muweze kujibu mapigo hayo baada ya
kujipanga kwa hoja na vifungu vitakavyoingia hatimaye kwenye katiba ya nchi hii.
Binafsi sioni sababu ya nyie kwa elimu na ujuzi wenu:
i. Kukosa kutambulika, heshima na tunzo za juu za kitaifa;
ii. Kulipwa mishahara mizuri kuliko Mameneja wageni (walioulia mbali
mashirika ya umma na yale yaliyobinasishwa) na Wanasiasa wa nchi hii na
kwanini wanasiasa hao hususan wabunge wasilipwe kutokana na elimu na ujuzi
wao tu;
iii. Mdai uhuru wa kuendesha mashirika na makampuni kama watu uhuru
bila kuyumbishwa na wanasiasa daima;
iv. Kuweza kufikia kilele cha mafanikio yenu kupitia kazi yenu ikiwemo
katika kipato, elimu, ujuzi na mchango wenu kwa taifa bila kulazimika kuwa
wanasiasa;
v. Kukubalika kwa nafasi yenu iwe mmo katika mashirika ya umma au
mashirika binafsi kama viongozi wa Kiuchumi katika nchi yetu.
HakiKatiba 2011
No comments:
Post a Comment