Friday, May 27, 2011

26. Mvuvi

MTANZANIA wewe ndiye unayemwajiri rais, mawaziri, wabunge na watumishi wa

umma. Na wewe ndiye mmiliki wa Katiba. Na katiba ni mchakato wa wewe

kuwaambia watawala waliopo na wajao unataka utawaliwe vipi na wao. Je, kuna

mtu mwingine anayeweza kuwasilisha ipasavyo unachokitaka kiwe, matakwa yako,

matarajio yako maslahi yako na ndoto ya Tanzania uitakayo na ile ya wewe

mwenyewe unachotaka kuwa kama sio mwakilishi wako anayeguswa na

yanayokugusa?

Tanzania bado ina uvuvi wa enzi za Sultan Barghash. Ipo haja ya wavuvi kuja na

hoja ya kuitaka serikali kutoka na mipango, mkakati, sera na mwongozo wa Uvuvi

Kwanza kwa niaba ya wakazi wa maeneo karibu na maziwa na bahari. Mkakati

utakaowawezesha wavuvi kuanzisha vikundi vya kijamii (CBOs) au ushirika

kuufanya uvuvi kuwa wa kisasa na wenye tija na faida kwao.

Na wavuvi hawawezi kufanikiwa katika hili bila kilio na matarajio yao kufikishwa

kwenye Baraza la Katiba Mpya 2011 na matakwa yao kuzungumziwa kwa ufupi

ndani ya katiba na kirefu katika sheria, miipango na sera zitakazotengenezwa

baada ya kutoka kwa Katiba Mpya.

No comments:

Post a Comment