HAPA tuwalenge waandishi wa habari ambao ama wanatumiwa na serikali katika
vyombo vya serikali ambavyo vilistahili kuwa vya umma na wale wanaotumiwa na
wanasiasa katika vyama vya upinzani.
Cha kushangaza ni kuwa serikali na chama tawala vimekuwa vinatumia wakati
wake mkubwa kuonya kuwepo kwa udini nchini lakini vinashindwa 'kuaddress'
hasa kinachoweza kuwa chanzo kikubwa cha udini nchini nacho ni vyombo vya
habari na waandishi wa habari kama tulivyoona Rwanda, C'ote d'Ivoire na
kwingineko Afrika.
Tunapozungumzia TBC au Daily News au Habari Leo ni lazima vyombo hivi vya
habari kwanza, kabla ya yote, viwe ni vya umma na sio vya serikali. Hili likifanyika
Wakurugenzi na Wahariri wa vyombo hivyo hawatatishwa au kutumiwa au
kutumika na viongozi wa serikali na chama tawala kwa maslahi yao. Vyombo hivyo
vitakuwa huru na ambavyo vitafanya kazi bila kumuonea au kumpendelea mtu au
chama au upande wowote kutokana na shinikizo za ndnai na nje ya chombo
husika.
Na sisi waandishi wa habari tunahitaji kujipanga na kukataa kutumika kama
changudoa kutokana na ule ukweli wenye kututumia wana ajenda zao. Na ajenda
hizo zinaweza kuishia kutupeleka na sisi kwenye Mahakama za Taifa kama
waangamizaji watu na nchi zetu. Tuwe makini.
Kwa hiyo ni muhimu sana kuwepo na Baraza au Mkutano wa Kitaifa wa Katiba
Mpya 2011 ili sisi waandishi wa habari tuwasilishe barazani humo jinsi
tunavyoamini nchi iendeshwe ili vyombo vya habari kama ilivyo Marekani au
Uingereza kweuli uwe ni mhimili wa nne wa kutegemea katika jengo la ghorofa
ndefu la demokrasia na haki ya binadamu tuliloanza kulijenga kimashamashaka
ifanyike kwa ari kuu, wito na dhati ya moyo na matendo.
HakiKatiba HATUTAWEZA kuvifufua na kuviendesha viwanda vya mafanikio bila mchango wa Wahandisi wetu wenyewe!
No comments:
Post a Comment