Friday, May 27, 2011

2. MFANYAKAZI SEKTA BINAFSI.

MFANYAKAZI wa sekta bnafsi sekta inayochukua nafasi ya ile ya umma anahitaji

pia kuwezeshwa ili isionekane kwamba sikuzote Mtanzania ni mtu wa kunyonywa,

kunyanyaswa na kudharauliwa tu.



Mfanyakazi huyu ni lazima alipwe mshahara unaoweza kukimu mahitaji yake yote

ya msingi na kudunduliza akiba kwa ajili ya dharura na mahitaji yanayokuwa

kutokana na kukua kwa familiaa.



Hali ilivyo sasa ni kuwa hata wale wafanyakazi wa tabaka la pili ambao juzi na jana

walikuwa na uwezo wa kubeba gharama za utunzaji na uendeshaji chombo cha

usafiri hivi leo wana tishio la kushindwa kumudu kutunza magari yao.

Ukija hilo daraja la chini hali ndio mbaya kabisa na katika nyumba nyingi lishe ni

duni, fedha sikuzote hamna na mahitaji mengi ya msingi ni vita kuyamudu.



Jitayarisheni, jiandaeni na kujihami na nguvu za hoja kuhusu umuhimu wa kuwa

na Baraza au Mkutano wa Kitaifa wa Katiba Mpya 2011 na wala sio Tume au

Kikundi cha wateuliwa wachache hata kama ni mawaziri, wabunge, majaji,

wanasheria na engineo kama hao, maana historia inaonesha wote hao hawawezi

kutetea maslahi yako wewe na kwamba mwamba ngoma ngozi lazima avutie

kwake au sio?



HakiKatiba 2011: Mfanyakazi kamili ni yule ambaye anatimiziwa mahitaji yake yote ya msingi. Na mwajiri adilifu ni yule anayejua kuwashibisha kwanza wafanyakazi wake kabla yeye mwenyewe hajala.

No comments:

Post a Comment