MTANZANIA una haki ya wewe kuwa na mwakilishi katika chombo kitakachozungumzia na kisha kusaidia kazi ya kuandika katiba mpya. Katika wakati huu, wewe mwananchi, raia wa Tanzania unapanda cheo na kuwa ndiye mwajiri wa rais,makamu wa rais, mawaziri, wabunge na watumishi wote wa serikali. Kazi yangu katika mchakato huu ni kuwaambia viongozi hao kwamba: 'tunawataka mtutawale hivi na uwezo na sifa zenu ziwe hivi. Kinyume cha hivyo tutawafuta kazi..' endelea kurasa inayofuatia:
Friday, May 27, 2011
5. MWALIMU.
MWALIMU kwenye miaka ya 1960 mara tu baada ya mkoloni kuondoka
walipendwa, kuaminiwa na kuheshimika lakini sio leo.
Je, tuanwezaje kurudisha upendo, imani na heshima kwa walimu hapa Tanzania?
Kilichofanyika hadi kufikia hapa ni kwamba wanasiasa waliamini kwamba wao ndio
wanaostahili kulipwa mishahara mizuri kuliko walimu wetu. Na kwamba ualimu si
kazi ya maana, wanaotaka waingie na wasiotaka watoke kirahisirahisi tu.
Matokeo yake ndiyo hayo ya kuporoka kila siku viwango vya elimu iwe ni msingi,
sekondar au high school!
Usahihishaji mitihani ndao unakuwa wa kibabe, kinuni na unaochangia
wasahihishaji kuondoka na zigo la madhambi kwa sababu ya kukosa kutenda haki
kwa watahiniwa. Hivi leo anayetegemewa kufaulu anaweza akafeli na mtu wa
kufeli akafaulu eti kwa sababu za kiufundi au kiteknohama. Lakini ukweli ni kuwa
upo uwezekano mkubwa wa haki sasa kununuliwa na wengine kudhulumiwa.
Tatizo ni mfumo wa usahihishaji uliopo ambao hauna wakati mwingine 'local
external examiner' na 'external examiner' kutoka nchi za nje ili kukamata uhalifu
huu katika 'sampling' itakayofanyika kiufundi na kijanja.
Lakini pia malipo kwa wasahihishaji yanapokuwa kidogo au wanapokuwa
wanapunjwa na maofisa husika au wanapokosa hazi zao nyingine kama wasahihi
shaji hili ni jambo la kutegemewa.
Lakini kubwa zaidi ni lile la kutaka kuitawala nchi nzima kutoka Dar es salaam.
Ninaamini kwa wingi wa shule tulizonazo leo wakati umefika wa kuwa na Bodi za
Mitihani za Mikoa ambazo zingeliandana uzuri sana na lile wazo la kuwa na
serikali huru kiuchumi na kijamii za mkoa. Mitihani itakaposimamiwa katika ngazi
ya mkoa au kanda kwa kuanzia itarahisisha usahihishaji wake na matumizi ya
wasahihishaji/waangalia mitihani toka mikoa mingine na nchi za nje.
Lingine ni lile la kurudisha MItihani yetu yote katika nchi zetu za Afrika Mashariki
iwe chini ya Bodi moja ya Mitihani ya Afrika mashariki kama ilivyokuwa East
African Cambridge enzi hizo!
Jitayarisheni, jiandaeni na kujihami na nguvu za hoja kuhusu umuhimu wa kuwa
na Baraza au Mkutano wa Kitaifa wa Katiba Mpya 2011 na wala sio Tume au
Kikundi cha wateuliwa wachache hata kama ni mawaziri, wabunge, majaji,
wanasheria na engineo kama hao, maana historia inaonesha wote hao hawawezi
kutetea maslahi yako wewe na kwamba mwamba ngoma ngozi lazima av
utie kwake au sio?
HakiKatiba 2011 Nchi isyowathamini na kuwalipa mishahara mizuri maprofesa, wahadhiri na walimu wake na badala yake ikakufuru kuwalipa wabunge, wanasiasa na viongozi wa serikali vizuri kuliko kundi hili na mengine kama haya lisahau kabisa kuondokana na umaskini, ujinga, maradhi na kuwa nyuma kimaendeleo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment