Thursday, May 26, 2011

46.. MWANAMTAA.

JE, unajua wewe ndiye MMILIKI WA KATIBA na ndiye unayemwajiri rais, makamu wake, mawaziri na serikali nzima ?

Na unajua serikali za mitaa zinazoruhusu kupigwa kelele majiani na kujengwa mabaa, madisko na mapabu karibu na watu wanakoishi au sehemu za Ibada au hospitali na maeneo kama hayo zinavunja sheria na katiba ya nchi? Na wanaowalinda wanaovunja sheria hizi ni mhaini na mchozhezi mkubwa katika jamii na amani na utulivu wake?

Watanzania tunastahili kabisa kwa heshima na taadhima ya Utanzania wetu kuwa watru wa staha, kuona aibu kufanya mambo fulani karibu na makazi ya watu pamoja na sisi kuwa watu wavumilivu na wastahimilivu kwa wenzetu wanaokwenda upogo.

Lakini haya makampuni yenye kutaka kutupasua ngoma za masikio kwa makelele ya promosheni mitaani tutazielewa vipi?

Na tutamwelea vipi huyu bwana anayefungua baa na akachoma nyama ya nguruwe karibu na Msikiti wa Waislamu tena kwenye mkoa ambao kimsingi ni wao? Hivi anamtakia nani mema, maana hata yeye mwenyewe sidhani kama anajitakia mema.

Tutamwelea vipi huyu dada anayefungua 'disco' au 'pub'
jirani na shuel au hospitali? Hawa kweli wanajua wanchokifanya.

Na tutawaelewa vipi pia hao wanaowapa ruhusa ya kufungua au kujenga baa, magesti, disco na pub katika maeneo kama hayo. Hivi kweli hii ndiyo kazi ya meya na madiwani?

Sio muhimu kweli kujipanga na kupanga miji yetu ili baa,disco na mapub yawe mahala pake na mahala pa kuishi na kulala pawe tofauti?

Sio busara na hekima tupu kuhamisha mabaa, kitimoto na magesti yaliyoruhusiwa karibu na makanisa, misikiti na shule tena za msingi?

Nani atakusaidia katika hili mwanamtaa kama na wewe hutokuwa na sauti katiba Baraza la Katiba Mpya Tanzania 2011?

No comments:

Post a Comment