Friday, May 27, 2011

19. MBUNGE, MWANASIASA.

BILA kufungwafungwa na ubinafsi, umimi na uchama tujiulize maswali haya:

i. Nini nafasi ya mbunge katika nchi inayotaka kujenga demokrasia na

kudumisha haki za binadamu (tofauti na maneno ya kiongozi wa chama fulani

anayedai eti mfumo wa vyama vingi uliletwa na IMF na sio Watanzania.) na kulea

kukuza hulka ya ushindani na maisha ndani ya jamii inayokubali tofauti zake lakini

ikaishi kwa kushirikiana katika kujenga taifa bora na madhubuti zaidi kiuchumi,

kijamii, kisiasa, kiutamaduni na kiteknolojia?

ii. Je, wakati haujafika wa kuwa na Tume huru ya uchaguzi hata kabla ya

mchakato wa Katiba Mpya haujaanza?

iii. Je, kisheria na kikatiba hatuoni 'tumejikwaa' tunapokataa kuwepo kwa

Mgombea huru nchini kwetu.

iv. Je, baadhi ya kanuni na misingi ya kukubaliana ndani ya chama hata

kama kuna makosa makubwa yanatendeka haijapitwa na wakati. Na sio vyema

kuruhusu waziwazi migogoro ndani ya chama ili kukisaida chama kuwa bora zaidi.

v. Nini uwe uhusiano wa rais na serikali kwa upande mmoja na wabunge,

watumishi wa umma na wanasiasa kwa upande mwingine.

vi. Nini kiwe kiwango cha chini cha elimu ya mwanasiasa ili viongozi wa

chini wawe na elimu, uwezo na maarifa ya kuongoza vyema kuliko ilivyo hivi sasa

?

vii. Nini kifanyike ili wabunge wasiwe mateka wa serikali na vyama vya

kisiasa katika kufanya maamuzi yao ? Kwa maneno mengine wabunge wasiwe

wanalindwa na serikali au chama cha siasa bali walindwe na nguvu na heshima ya

bunge la Jamhuri ya Tanzania na ikiwezekana kuwe na bunge la pili kudhibiti

shughuli kwa kiasi fulani kati ya wabunge hawa na serikali yao na mkuu wa nchi?

viii. Kwanini tusiwe na Chuo Kikuu kinachofundisha kwa Kiswahili ili angalau

madiwani wetu, wenyeviti serikali za mitaa, makatibu kata na viongozi katika

matawi ya vyama huko chini wapate digrii ya kwanza, ya pili na ya tatu kwa

kiswahili katik masuala ya uchumi, menejimenti na uongozI?

ix. Je, wakati haujafika kwa wabunge na wanasiasa kuangalia uwezekano

wa kuwa na serikali huru kiuchumi na kijamii kimkoa ili kuufikisha uongozi karibu

zaidi na wananchi kuliko ilivyo sasa. Serikali huru kiuchumi na kijamii za mikoa

zitakazoruhusu kuwepo kwa Waziri Mkuu, mawaziri wa mkoa na wawakilishi wa

bunge la mkoa ambao kazi yao kubwa ni kuhakikisha kwamba maendeleo ya

kiuchumi na kijamii katika mkoa hayavurugwi na serikali kuu. Aidha, rasilimali na

mali asili za kila mkoa kutumika kwanza kwa manufaa ya wakazi wa mkoa husika

tofauti na ilivyo sasa. Serikali ambazo pia zitaweza kupata ushirikiano na misaada

toka nje moja kwa moja?

x. Je, hakuna umuhimu wa kuwepo na chombo huru nje ya serikali na

vyama vya kisiasa ili kuhakikisha kuwa katiba na sheria za nchi zinafanya kazi na


WATAKAOCHANGIA bila uchama, ukabila, ueneo, udini, ubinafsi na ushawishi wowote toka kundi lolote ndani au nje ya nchi watastahili kupewa tunzo ya juu kabisa ya Kitaifa.

NI haki na wajibu wenu pia kuwaamsha, kuwafundisha na kuwaelekeza wananchi wengine nini wanachopaswa kufanza ili mahitaji yao ya msingi, dhiki, mapungufu kwao, kasoro zilizopo kwenye maeneo na maisha yao, haki na maslahi yao yote yaweze kupatikana kwa kutumia katiba na sheria za nchi na sio vinginevyo.

Ni muhimu pia wananchi kuelewa kwamba serikali ni kitu kinachodumu milele mpaka mwisho wa dunia lakini vyama vya kisiasa ni taasisi za kupita, leo vinaweza kuwepo na kesho visiwepo na vikaja vyama vipya kabisa madarakani.


wanaokosea kukosolewa na kuchukuliwa hatua zifaazo?

No comments:

Post a Comment