MTANZANIA una haki ya wewe kuwa na mwakilishi katika chombo kitakachozungumzia na kisha kusaidia kazi ya kuandika katiba mpya. Katika wakati huu, wewe mwananchi, raia wa Tanzania unapanda cheo na kuwa ndiye mwajiri wa rais,makamu wa rais, mawaziri, wabunge na watumishi wote wa serikali. Kazi yangu katika mchakato huu ni kuwaambia viongozi hao kwamba: 'tunawataka mtutawale hivi na uwezo na sifa zenu ziwe hivi. Kinyume cha hivyo tutawafuta kazi..' endelea kurasa inayofuatia:
Friday, May 27, 2011
6. MHADHIRI, PROFESA.
UKIKUTANA na maprofesa wetu ambao walikuwa wakimuogopa Mungu na kuishi
kimaskini kwa tumaini kuwa mishahara na pensheni zao zingeliwasaidia uzeeni,
aghalabu utatamani kulia.
NI maprofesa na wahadhiri ambao walimwibia mwajiri wao muda au kutumia utafiti
au ushauri kujitajirisha wao binafsi ndio wenye maisha mazuri.
Ipo haja ya kuangalia upya mishahara ya maprofesa na wahadhiri wa vyuo vikuu ili
tupate kilicho bora kutoka kwa na wanafunzi wao. Hivi leo, kwa kiasi kikubwa ni
kwamba tunajidanganya kwamba tunawalipa na wao wanadanganya wanatimiza
wajibu wao.
Njia mojawapo ya kuongeza mishahara na marupurupu ya wasomi hawa ni
kuhakikisha vyuo vikuu vinakuwa na miradi mizuri na toshelevu na endelevu
itakayoingiza kipato cha ziada kitakachotumiwa kwa maslahi ya walimu na
wafanyakazi wengine wa vyuo vikuu, kwa mfano, katika masuala ya kodi za
nyumba, usafiri na manunuzi ya vitabu na visaidizi vingine vya elimu na kisomo.
Namna nyingine ya kuongeza kipato kwa wafanyakazi wa vyuo vikuu vyetu ni
kuvitengea bajeti tosha ya utafiti kazi ambayo itafanywa na wote, walimu kwa
wanafunzi na mwisho wa siku wote watanufaika na kupunguza sana kilio cha
kipato na maslahi. Hili lal utafiti linaendana na matumizi ya ushauri wa walimu na
maprofesa wa vyuo vikuu badala ya serikali zetu kushauriwa na watoto wa mjini au
watumishi wa umma wakiwemo makatibu wakuu na mawaziri wenyewe kufanya
mipango ya kuwa na washauri wa kupanga toka ndani na nje ya nchi.
Endapo kila Mkoa nchini utakuwa na Chuo Kikuu chake cha umma, mishahara na
maslahi ya maprofesa na wahadhiri yana uwezekano mkubwa zaidi wa kuwa bora
na ya kuridhisha zaidi kwa sababu kwanza watakuwa kwenye mikoa ambayo si
ghali kama Arusha, Mwanza, Dodoma na Dar es salaam.
Sio tu kipato na maslahi ya maprofesa na wahadhiri yataongezeka bali hata
maendeleo ya kielimu, kijamii, kiuchumi, kiutamaduni, kisiasa na kiteknolojia ya
mikoa husika itakwenda kwa kasi zaidi kuliko ilivyo hivi sasa.
Na hili linawezekana kwa kuwatumia maprofesa na walimu waliopo hivi sasa na
kugawanya vitivo au fani za masomo mbalimbali ili Chuo Kikuu kimoja kisiwe na
zaidi ya fani 2-3 tu!
Isitoshe kuna maprofesa na wahadhiri wengi tu wasio na kazi kwenye nchi za
Ulaya Mashariki, Urussi na jamaa zake, Ireland, Spain, Portugal na hata Marekani
kwenyewe.
Yote haya yanaweza tu kufanikiwa ikiwa ni wahadhiri na maprofesa wenyewe ndio
watakaokuwa wawakilishi katika Baraza au Mkutano wa Kitaifa wa Katiba Mpya
2011.
HakiKatiba 2011 Nchi isyowathamini na kuwalipa mishahara mizuri maprofesa, wahadhiri na walimu wake na badala yake ikakufuru kuwalipa wabunge, wanasiasa na viongozi wa serikali vizuri kuliko kundi hili na mengine kama haya lisahau kabisa kuondokana na umaskini, ujinga, maradhi na kuwa nyuma kimaendeleo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment