Friday, May 27, 2011

25. Msanii, Mwanamuziki.

MTANZANIA wewe ndiye unayemwajiri rais, mawaziri, wabunge na watumishi wa

umma. Na wewe ndiye mmiliki wa Katiba. Na katiba ni mchakato wa wewe

kuwaambia watawala waliopo na wajao unataka utawaliwe vipi na wao. Je, kuna

mtu mwingine anayeweza kuwasilisha ipasavyo unachokitaka kiwe, matakwa yako,

matarajio yako maslahi yako na ndoto ya Tanzania uitakayo na ile ya wewe

mwenyewe unachotaka kuwa kama sio mwakilishi wako anayeguswa na

yanayokugusa?

Tanzania ina kila sababu ya kuongoza Afrika katika muziki, ngoma, filamu, redio,

telelvisheni, magazeti, michezo ya kuigiza na maeneo yote ya sanaa na muziki

endapo tu viongozi wetu watakuwa mstari wa mbele kwenda kufanya kazi kule

wananchi waliko na sio kujifungia kwneye maofisi yao yenye viyoyozi kule Dar es

salaam.

Tunapozungumzia mafanikio ya sekta hii hakika tunazungumzia mabilioni ya

shilingi yatakayotiririka kwenye hazina ya taifa na kuipunguzia nchi umaskini, elimu

duni na tiba zisizoridhisha za afya. Aanayechezea namna hii shilingi chuoni hivi

anafaa kuwa kiongozi wa Watanzania?

Ni lazima tuoneshe njia kwa kushiriki katika Baraza la Katiba Mpya ili serikali iwayo

ijue tunataka sekta yetu ya muziki na usanii iendeshwe vipi na sio kwa huruma na

msaada wa huyu au yule ambaye hatakuwa nasi au na kizazi chetu kijacho daima.

No comments:

Post a Comment