JE, unajua wewe ndiye MMILIKI WA KATIBA na ndiye unayemwajiri rais, makamu wake, mawaziri na serikali nzima ?
Watoto nao wana madai mengi:
. Hawana kwanza viwanja vya michezo na katiba lazima ilipitishe hili na hali kamwe isiwe kama ilivyo leo kwa kuwa na mipango madhubuti vijijini na mijini;
. Hawalindwi wakiwa nyumbani au barabarani;
. Wana chakula na lishe duni inayochangia wengi kukosa akili darasani kwa kukosa protini inayopatikana kwenye maharagwe, karanga, samaki, nyama, mayai na maziwa;
. Hawana vifaa vya michezo na toys 'wansesere' wa kutosha na wengi wao wanachezea vitu vya ajabu ajabu ikiwemo katika baadhi ya mikoa watoto kuchezea mabomu au sumu;
. Michezo wanayoipenda watoto kama vile kuogelea au kukimbia au kuendesha baiskeli ni migumu na ghali kushriki na wengi wanaangukia kwenye utundu ulio hatari kwa maisha na hasara kwa wazazi wao;
. Watoto wanapogundua kitu kwa mfano kigari, mfumo wa kuwasha taa wa umeme; redio inayozungumza kweli; kurusha matangazo ya reio; kompyuta la maboksi; mchezo fulani au sanaa fulani au mashine au mtambo wa hiki au kile wazazi, wahandisi na serikali yao badala ya kuwasaidia kukuza vipaji hivyo na kuwageuza wazalishaji kitu fulani huwagandamiza na kuwasambaratisha na kuwaharibia kabisa maisha yao.
. Watoto wanabwaka na kunajisiwa ovyo;
. Katika baadhi ya shule kuna wanafunzi zaidi ya 100 katika darasa na hivyo hakuna mwalimu anayeweza kuwatendea haki wanafunzi dhaifu na walio nyuma kimasomo;
. Daladala na hususan zile za Dar es salaam zinawanyanyasa wanafunzi kupitukia na sio kupindukia tu vikionesha jeuri yao kama vile zinamilikiwa na wenye serikali wenyewe. Ni ndoto ya kila mwanafunzi Dar es salaam kwenda na kurudi toka shule bila kubughudhiwa au kunyanyaswa ili changamoto yake ibakie tu ni kujifunza na sio kujilinda tokana na unyanyasaji huu;
. Wakati nchi nyingine zimegawa kompyuta za bei rahisi kwa wanafunzi wote wa shule za msingi watoto wanashangaa kuiona Tanzania pamoja na utajiri wake wa almasi, dhahabu, Tanzanite na madini mengine inashindwa kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment